MISSIONARY SISTERS OF THE PRECIOUS BLOOD EAST AFRICAN PROVINCE
Shirika la Masista wa Damu Azizi ya Yesu au Damu Takatifu walifika Jimboni Tanga walitokea Afrika ya Kusini mwaka 1898. Kwa hiyo mwaka 2008 Masista hawa hawa wanatimiza miaka 110 ya utume wao Tanga.

Mwanzilishi wa Shirika la Masista wa Damu Takatifu ni Abate Francis Pfanner ORC. Alianza kazi ya umisionari Afrika ya Kusini mwaka 1880. Mwaka 1885, wakandidati watano walijiunga hivyo hao wakawa Masista wa kwanza katika Shirika. Lengo la mwanzilishi lilikuwa ni kuunda Shirika litakalo eneza Injili kwa kazi mbalimbali hasa kulea na kuwafundisha vijana, kuwahudumia wagonjwa na kazi nyinginezo.

Jinsi Masista walivyoongezeka, shirika liliimarika. Mwaka 1902, Baba Mtakatifu Pius wa Kumi aliidhinisha hati ya Shirika kwa kuitia saini.

Kazi zao walizofanya tangu wafike Tanga mwaka 1898 ni kutoa huduma Maparokiani, Kufundisha Mashuleni, kutoa mafunzo ya Ufundi na kutoa huduma za Afya. Walianzisha Shule ya Kifungilo mwaka 1935. Ilianza kama kituo cha kutunza watoto, baadaye ikawa shule ya Msingi, baadaye mwaka 1981 ilianza kutoa masomo ya Sekondari ikijulikana kama Shule ya Sekondari ya Wasichana Kifungilo. Mwaka 1996 kidato cha tano na sita kilifunguliwa.

Masta wa Damu Takatifu pia hutoa huduma katika Majimbo mengine. Haya ni Arusha, Moshi, Morogoro, Zanzibar na Nairobi. Pia hutoa huduma nchi za Zambia, Zaire, Zimbabwe, Afrika ya Kusini, Korea, Amerika, Kanada na Ulaya.

Nembo yao ni Mwana Kondoo wa Pasaka, Mkombozi wetu aliyekuwa tayari kujitolea kwa ajili ya wanakondoo.