Rosminian Fathers (I.C), Brothers

Shirika la Mapendo lilianzishwa mwaka 1828 na Mwenye Heri Antonio Rosmin. Huyu alikuwa Mwana Falsafa liyejulikana sana. Mwaka 1932, nyumba ya Malezi ilianzishwa huko Ireland. Nyumba hii ikawa chachu ya Miito mingi. Mwaka 1938 Chuo kilichopewa jina la Rosmini kilifunguliwa huko Roma. Jumuia ya Warosmini ilianza kukua. Walifanya kazi huko Thailand. Mwaka 1942 walishauriwa kuelekeza utume wao Barani Afrika. Kwa kupitia Vikarieti ya Kilimanjaro chini ya Mhashamu Askofu Joseph Byrene hatimaye mwaka 1945 Warosmini wakwanza waliingia Tanganyika. Wawili kati yao ni Pd. Walter Dich na Pd. Francis Kennedy.

Warosmini waliofika Kilimanjaro walipewa kwanza jukumu la kufundisha Chuo cha Singachini huko Moshi. Pd Walter akawa Mkuu wa Chuo. Mapadre wengine walifuata baadaye. Mhashamu Askofu Joseph Byrne aliwatuma Warosmini wafanye kazi Tanga. Hatimaye Pd. Eugen Arthurs aliteuliwa kuwa Prefekti wa Kitume Tanga ilipokuwa Prefectura, na baadaye akawa Akofu wa Jimbo la Tanga mwaka 1958.

Makao makuu ya Shirika la Warosmini katika Afrika Mashariki yapo Mwambani hapa Tanga. Makao makuu Kiulimwengu ni Monte Calvario huko Domodossola katika kingo za Milima ya Alps kwenye mpaka kati ya Italia na Uswisi. Shirika hili limesambaa mahali pengi Duniani.

Warosmini wamefanya kazi kubwa za Kichungaji hapa Jimboni Tanga. Parokia nyingi za Jimbo zimeanzishwa na Warosmini. Hadi sasa hivi wanasimamia parokia kadhaa Jimboni. Baadhi ya Parokia hizo ni Gare, Kwalukonge, Mombo, Saruji, Lushoto na Kwai. Wanazo nyumba za malezi ya vijana huko Lushoto na Gare. Pia wanasimamia Shule ya Sekondari ya Rosmini ambayo zamani ilijulikana kama Saruji.

Pamoja na kufanya kazi kubwa ya kichungaji kwa zaidi ya miaka hamsini hapa Tanga, Shilika hili halikufanya jitihada za kutosha kuvutia vijana wengi kutoka Tanga kuupenda wito wa Upadri katika Shirika lao. Hadi sasa, vijana waliopewa Daraja Takatifu la Upadre kutoka Tanga ni wachache ukilinganisha na muda wa uchungaji waliofanya hapa tanga..

Benedictine Fathers (OSB) and Brothers

Wamonaki wa Kibenedictini wa Mtakatifu Ottilien walikuja kusini mwa Tanzania tamgu mwaka 1887. Walianzisha nyumba yao huko Ndanda. Mwaka 1946 walipata nyumba ya mapumziko katika Milima ya Usambara. Sehemu hii ya Usambara ilikuwa ni shamba la Mjerumani aliyejulikana kwa jila la Sakharani ambalo lilisheheni zao la kahawa na miti ya aina mbalimbali. Eneo hili liliitwa Sakharani au Sakarani kumuenzi aliyekuwa mmiliki wa Shamba hilo:

Chaple
Wamonaki watatu waliofika mwanzoni ni Pd. Edward Wildbaher, Br. Fintan Frank na Br. Fortunatus Mayer. Hali ya hewa ya Sakharani ni baridi ambayo ni karibu sawa na ile ya Ulaya, hivyo sehemu hii ikawa sehemu nzuri ya mapumziko.

Mwaka 1970, Padre Burkad alifika Sakharani. Yeye aliomba kibali cha kufanya kazi za Kichungaji katika maeneao ya Masange na maeneo yanayoizunguka Sakharani. Aliweza kujenga Parokia ya Sakharani na vigango vyake, yaani, Kwehangala, Tekwa, Baga, Kwesine na Msamaka. Baadaye mwaka 2001 kigango cha Tekwa kilifanywa kuwa Parokia chini ya Padre Joseph Sekija. Baadaye Padre Edwin alifika na kusaidia kazi za Kichungaji.

Padre Beda Pavel alikuwa Mwalimu huko Soni Seminari wakati ilipoanzishwa. Padre Odillo Huppi alianzisha Parokia ya Handeni na utume rasmi kwa Wamasai. Padre Damian Milliken ameanzisha Shule ya Sekondari ya Wsichana Mazinde Juu na ujenzi wa Kanisa la Mabughai ambalo lina hadhi ya kuwa Parokia.

Padre Athanas Meixner alipewa jukumu la kuanzisha Parokia huko Soni na aliifanya kwa ufanisi. Pia amesaidia ujenzi wa Kanisa la Manundu -Korogwe na Kanisa la Malindi. Pia ameanzisha shamba huko Kwematuku -Korogwe.

Pamoja na kazi za Kichungaji zilizofanywa na Wamonaki hawa, kazi zao kuu hasa ilikuwa ni kilimo, ufugaji na ufundi. Walizanza kwa ujenzi wa nyumba na mabanda ya ngombe. Pia waliendeleza mashamba ya kahawa na miti ya quinine. Wamonaki hawa walisaidia sana katika ujenzi wa makina na nyumba mbalimbali za Kanisa. Br. Fortunatus atakumbukwa sana kwa mchango wake wa ujenzi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Anthony Tanga.

Katika viwanda Wabenedicti wameazisha kiwanda cha kutengeneza divai na kutengeneza mafuta ya kadamia. Pia wanayo karakana ya seremala na magari, upo ukataji wa mbao na utengenezaji wa siagi.

Wamonaki Wakibenedicti wamejitahidi sana kulea Miito ya Upadre na Kitawa. Padre Ernest Seng’enge, Padre Antony Mtunguja, Clement Kihiyo Jandu; Padre Placidus Mtunguja (OSB), Padre Cornelius Mdoe (OSB), wote hawa ni matunda ya utume wa Wabeneditini.

Bethlehem Missionary Fathers

Capuchin Fathers

Passionist Fathers

OSS Fathers