KANISA KATOLIKI TANGA

this page in english

Askofu Anthony M. Banzi, 1994 -

 

Matukio na picha

 

Mhashamu Askofu Anthony Banzi, alizaliwa tarehe 28th October, 1946 katika kijiji cha Mangoja, Parokia ya Tawa, Morogoro. Alipata elimu ya msingi katika shule msingi ya Lukenga. Mwaka 1960 alijiunga na Seminari ndogo ya Mt. Peter, Bagamoyo na baadaye Seminari ndogo ya Mt. Charles huko Itaga kuanzia mwaka 1965-1967.

Mwaka 1968-1969 alijiunga na Seminari Kuu Kibosho kwa masomo ya Falsafa na baadaye Seminari kuu Kipalapala kwa masomo ya Teolojia kuanzia mwaka 1970-1973. Alipewa daraja la upadre tarehe 29 Julai, 1973. Aliteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga tarehe 24th Juni, 1994 na kuwekwa wakfu tarehe 15th September 1994.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Askofu wa Tanga, alifanyakazi kama paroko msaidizi katika parokia ya Mlaki, Msongozi, Mtombozi, Matombo na kama Paroko katika Parokia ya Maskati. Mwaka 1976 alifanya kazi kama muhasibu mkuu wa Seminari kuu ya Ntungamo Bukoba. Mwaka 1976 - 1981 alikwenda Austria Ulaya kwa masomo zaidi ambapo alitunikiwa shahada ya udaktari (Ph.D). Kuanzia mwaka 1981 - 1982 alikuwa Chaplain wa Hospitali ya Turiani na pia paroko wa parokia ya Mandera.

Mwaka 1981 - 1985 alikuwa Mhasibu mkuu wa Jimbo Katoliki la Morogoro. Mwaka 1985 - 1987 alikuwa Chaplain wa Sekondari ya Bigwa Morogoro. Mwaka 1988 - 1991 alikuwa Gambera wa Seminari kuu ya Ntungamo. Mwaka 1992 Padre Anthony Banzi aliteuliwa kuwa Gombera wa seminari kuu ya Kibosho Moshi. ambapo alifanyakazi mapaka alipoteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo katoliki Tanga mwaka 1994.

Makazi ya Baba Askofu:
Bishop’s House, Raskazone,
P.O. Box 1108, Tanga.
Phone: Residence: +255-027-26242417
Ukiwa Tanga: 2642417.
Ofisini: +255-27-26242834.
Ukiwa Tanga: 26424117;
Fax: +255-27-26243548.
Ukiwa Tanga: 2643548
E-mail: bishopbanzi@gmail.com
Bishop's House - Raskazoni