KANISA KATOLIKI TANGA

this page in english

Mhashamu Askofu Telesphore Mkude, 1988 - 1993

 

Mhashamu Askofu Telesphor Mkude, alizaliwa tarehe 30 Novemba 1945 katika kijiji cha Pinde Parokia ya Mgeta Jimboni Morogoro. Alipewa Sacramenti ya Daraja Takatifu la Upadre tarehe 16 Julai 1972. Aliteuliwa kuwa Askofu wa Tanga tarehe 28 Januari 1988 na kuwekwa wakfu kuwa Askofu wa Jimbo la Tanga tarehe 26 April 1988. Tarehe 19 April 1993 aliteuliwa kuwa Askofu wa Morogoro na kusimikwa rasmi tarehe 13 Juni 1993. Hadi sasa yeye ni Askofu wa kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro.