KANISA KATOLIKI TANGA

KARISMATIKI

 

Karismatik Tanga ilianzianzishwa katika Kanisa la Mtakatifu Karol Lwanga mwaka 1994. Kikundi hiki kilianza na watu 15 waliojitolea. Baadaye Karismatik ilienea Parokia nyingine na kwa sasa inakaribia kufikia Parokia zote za Jimbo.

Kikundi cha Karismatik Duniani kisingeweza kukua na kuenea kama Mtaguso wa Vatikan usingejenga Roho ya Uwazi na Uvumilivu ndani ya Kanisa Katoliki wakati Kanisa likitafakari upya ni nini Roho anataka kusema

Malengo ya Karismatik ni:

v Kuimarisha ukomavu wa kumuongokea Yesu, Bwana na Mkombozi wetu.

v Kuimarisha maamuzi binafsi ya kuamini uwepo wa nguvu za Roho Mtakatifu.

v Kuimarisha upokeaji na utumiaji wa Mapaji ya Roho Mtakatifu “Karismata” si katika Karismatik tu, bali kwa Kanisa zima kwa ujumbla.

Kazi zao
Ø Hukutana mara moja au mbili kwa wiki kwa ajili ya masifu, kuabudu, mafundisho ya Biblia na kushirikishana Neno la Mungu.

Ø Kuandaa Kongamano la Roho Mtakatifu.

Ø Maombezi ya uponyaji na uokoaji kila Ijumaa katika Ofisi za Karismatik kuanzia saa 9:00 – 12: 00 alasiri.

Ø Kutoa huduma za ushauri.

Charismatic office, Tanga Chumbageni

Ø Kutembelea wagojwa

Ø Kusaidia enye shida

Ø Kusambaza vitabu na majarida ya mambo ya Kiroho.

Mipango ya baadaye ni kufikisha Karismatiki Parokia zote na vigango vyake, kufanya makongamano ya Roho Mtakatifu nje ya Tanga, kuhakikisha kwamba Wanachama wake ni Wakristo kweli na Wakarismatik kweli.