KANISA KATOLIKI TANGA

This page in english

WAWATA

 

WANAWAKE WAKATOKI TANZANIA

UTANGULIZI

WAWATA (Wanawake Wakatokiki Tanzania) huu ni umoja wa wanawake wakatoliki Tanzania. Hili ni tawi la WUCWO (The World Union of Catholic Women Organization) ambacho kinafanyakazi chini ya sheria ambazo zinakubaliwa na kanisa Katoliki Tanzania chini ya Baraza la Maaskofu Tanzania T.E.C (Tanzania Episcal Conference). Kauli mbiu ya chama hiki ni: kwa Upendo wa Kristu, Tutumikie na kuwajibika Hii pia ni salamu ya wanachama wanapokutana. Umoja huu ulianza rasmi Jimboni Tanga mwaka 1974 chini ya uongazi wa marehemu Padre Gerald Chilambo wakati huo akiwa ni Director wa Utume wa walei. Mwenyekiti wa kwanza kabisa wa umoja huu alikuwa Mama Eva Mpangala na katibu wake alikuwa Mama Emmy Mapunda.

Malengo ya WAWATA

1. WAWATA ni kiunganishi cha Wanawake Wakatoliki Tanzania kwa ajili ya kuendeleza mchango na ushiriki waa katika maendeleo ya Kanisa na jamii na kuwawezesha kuhimili mabadiliko ya Ulimwengu huu. Mchango wao ili kuufanya Ulimwengu uwe mahali pema ni muhimu.

2. WAWATA huhimiza nafasi ya Wanaweke katika Kanisa na jamii kuwa wabunifu na kurekebisha udhaifu uliopo na kugundua nafasi mpya zitakazo saidia kujitoa zaidi katika jumuia. Kufanyakazi kwa kushirikiana na kujali ili kuwa na familia bora Tanzania.

3. WAWATA inasisitiza mafundisho ya Kanisa ili kufikia maendeleo ya Kiroka kwa mtu binafsi na jamii kwa ujumla, malezi ili kulinda na kutetea mafundisho ya Kanisa hasa katika Ulimwengu huu ubadilikao sana.

4. WAWATA hufanya kazi kwa ukaribu na asasi nyingine zinazojishuhulisha na malezi ya Kiroho na uinjilishaji kupitia Jumuia Ndogo Ndogo za Kikristo, kuendeleza mchakato wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, kuwatoa Wanawake katika dimbwi la ukwandamizwaji na uonevu ili kuwe na usawa katika haki za msingi na nafasi sawa katika maamuzi.

Uanachama

WAWATA ni kwa Wanawake wote waliobatizwa katika kanisa Katoliki. Kimsingi, Wanawake wote Wakatoliki Tanzania ni Wanachama wa WAWATA, hata hivyo uanachama kamili huanzia kumi na nne na kuendelea.

Huduma za WAWATA katika ngazi ya Jumbo

¨ Mikutano: Wajumbe wa Kamati Kuu hukutana mara moja kila mwezi katika Jumapili ya tatu ya mwezi. Mikutano katika ngazi nyingine hufanyika kutokana na Katiba.

¨ Semina: Semina huratibiwa na kamati kuu, na hufanyika katika kanda kila baada ya miezi mitatu. Zipo kanda tatu, kanda ya Tanga, Korogwe na Lushoto.

¨ Huduma kwa wenye shida: Hii hufanyika katika ngazi ya Parokia, Vigangoni na katika Jumuia. Hutembelea wagonjwa hospitalini na majumbani, hutembelea yatima, wajane na wazee na kuwapatia mahitaji mbalimbali kama chakula na nguo, huwaombea na kuwapa moyo.

¨ Huduma kanisani: WAWATA wapo katika mstari wa mbele, hushiriki katika kwaya, masomo Kanisani, wengine ni wanachama wa vyama vingine vya Kitume kama vile Legio Maria, Karismatik, Moyo Mtakatifu wa Yesu, Mama wa Shauri Jema na vinginevyo. Vile vile husaidia malezi ya Utoto Mtakatifu. WAWATA hujitolea kusaidia kuandaa sherehe mbalimbali za kanisa hasa Krismas, Pasaka, Upadrisho na nyingine. Wamekuwa mstari wa mbele katika kupamba na mapishi katika sherehe hizo muhimu za Kanisa.

¨ Msaada kwa Soni Seminari: Hutembelea Seminari ya Soni mara kwa mara na kutoa misaasa ya hali na mali hasa fedha na chakula pamoja na kuwapa vijana moyo wa kuwa tayari kuyatoa maisha yao kwa utumishi Mtakatifu. Pia wameendelea kuwapa moyo vijana waliojiunga na Seminari kuu kila mara walipokutana nao na kuwaahidi sala zao.

¨ Mkopo: WAWATA hutoa mkopo kwa wanachama wake ili kufanya miradi midogo ya maendeleo. Lengo la mkopo huo ni kuanzisha miradi na kubuni nafasi za kazi zitakazo wezesha kuondoa umaskini na utegemezi.

¨ Matazamio: Ni kuwasaidia Wanawake Wakatoliki wote kuwa wanachama mahiri wa WAWATA katika kutekeleza malengo na nia za WAWATA ili kujitakasa wao wenyewe na kuwasaidia wengine kuupata Ufalme wa mbinguni.

“Kwa Upendo wa Kristo Tutumikie na Kuwajibika”. Hii ndio mbiu ya kila mwanamke Mkatoliki Tanzania na kuingineko ulimwenguni.