JIMBO KATOLIKI TANGA

Masista wa Mama yetu wa Usambara.

Sisters of Our Lady of Usambara (COLU)

Jubilei na nadhiri

Kwamndolwa
Chaplain house Kwamndolwa
 
CONGREGATION OF OUR LADY OF USAMBARA

Shirika hili lilianzishwa mwaka 1954 chini ya Sr. Willibalda Giesbers (CPS) akisaidiwa na Sr. Ambrosis Mollers. Shirika lilianzia huko Rangwi katika Milima ya Usambara. Eneo hilo lilikuwa likimilikiwa na Mlowezi wa Kijerumani.

Hali ya hewa ya Rangwi ni baridi kali hasa wakati wa kipupwe na masika. Kutokana na hali hiyo, ilionekana ni vema kutafuta sehemu nyingine yenye hali ya hewa nzuri itakayosaidia wale ambao wanashindwa kuishi Rangwi. Hatimaye Kwamndolwa-Korogwe ikapatikana. Sehemu hiii lilikuwa shamba la mkonge. Shamba hili lilibadilishwa na kufanywa shamba la matunda, ufugaji na mazao mengine. Ujenzi wa nyumba ulifanyika na baadaye Kwamndolwa ikawa ndiyo Makao Makuu ya Shirika. Pamoja na ujenzi wa nyumba za kuishi, Shirika pia limejenga Shule ya Chekechea na Kituo cha Afya hapo Kwamndolwa. Pia Shirika liliweza kupata Shamba huko Kididimo-Muheza na kujenga Kituo cha Afya. Mpaka sasa nyumba za jumuia ni Konventi ya Rangwi, Konventi ya Kwamndolwa, Kituo cha Kufundishia Montessori, Mtakatifu Anna-Nguvumali, Kurasini, Karanga-Moshi na zipo nyumba za Masista katika baadhi ya Parokia za Jimbo.

Mwaka 1952, Serikali ya wakati huo ililitoa eneo hilo limilikiwe na Kanisa. Mwaka 1953 Pd. Eugen Arthurs pamoja na baadhi ya Masista walianza kukaa hapo. Juhudi zilianza za kutafuta wakandidati. Hatimaye mwaka uliofuata walipata wakandidati na Shirika kuanza rasmi. Wakandidati wakwanza kujiunga ni Atanasia, Genovefa, Veronika,Yohana, Teresia, Regina, Gratiana, Eugenia, Sabiona, Yohana na Klementina.
Sr. Willibalda_ic

Mwaka 1958, nazili za kwanza ziliwekwa kwa mara ya kwanza hapo Rangwi. Masista hao walitumwa kufanya kazi kwenye Maporikaia mbalimbali wakianzia parokia ya Lushoto.

Uongozi wa Shirika ni kama ifuatavyo:

1. Mama Mkuu, 2. Mama Mkuu Msaidizi na 3. Washauri watatu.

Katika vipindi saba vya uongozi, Shirika limeongozwa na Mama Wakuu wanne kama ifuatavyo.

Kipindi cha kwanza mwaka 1954-1976 alikuwa Sr.Willibalda Giesbers,

kipindi cha pili 1976-1982 na kipindi cha tatu 1982-1988 alikuwa Sr. Inviolata Mndeme,

kipindi cha nne 1988-1994 na kipindi cha tano 1994-2000 alikuwa Sr. Maura Kimaryo,

kipindi cha sita 2000-2006 na kipindi cha saba 2006 hadi sasa ni Sr. Leonia Mdoe.

Kazi zao

Masista wa COLU wanajishuhulisha sana katika kutoa huduma Maparokiani ndani ya Jimbo na nje ya Jimbo. Huduma hizo ni pamoja na kutoa mafundisho ya Katekismu kwa watoto wanaojiandaa kupokea Sacramenti za Ubatizo na Kipaimara, Mafundisho ya ndoa, kufundisha dini katika Shule za Msingi na Sekondari, mapishi na usafi wa nyumba na mazingira. Huduma hizo zitolewazo Maparokiani zimekuwa mwanga na chumvi ya kuwavuta watu wengi wasio Wakristu kuupenda na kuingia Ukristu. Pia huduma za Masista huko Maparokiani zimekuwa kichocheo ya Miito ya Upadre na Utawa.

Sr. Inviolata Mndeme.

Inaonesha kuwa, Parokia zilizokaa Masista kwa muda mrefu ndizo zilizotoa idadi kubwa ya Mapadre na Masista. Mfano mzuri ni Parokia ya Gare ambayo imetoa Mapadre wengi Jimboni Tanga Sehemu ambako hakuna masista miito ya Utawa na Upadre ni duni sana. Kwa upole na ukarimu wao, Masista wamekuwa walezi wazuri na wakaribu wa watoto, hivyo kuwavutia kuyapenda maisha ya utumishi.

Hongereni Masista na mjitahidi kufikisha huduma zenu katika Parokia zote za Jimbo. Masista hutoa pia huduma ya Elimu kwa Shule za Msingi, Sekondari na hata Vyuo. Kwa hiyo, Serikali pia inafaidika na huduma hizi za kitawa katika asasi zake. Hutoa huduma za Elimu katika Shule za Kanisa Jimboni hasa Mazinde Juu, Kongei, Kifungilo na Rosmini. Masista wanacho Chuo cha ukatekista huko Rangwi. Kipo pia chuo cha mafunzo huko Montessori.

Sr. Maura Kimaryo

Pia Masista hujishughulisha na viwanda vidigo vidogo hapo Montessori, hivyo huzalisha siagi ya matunda, samli na divai ya ndizi. Hutengeneza pia viungo vingine vya chakula. Zaidi ya hayo, Montessori pia hutengeneza masweta ambayo yanahitajika sana kwa hali ya hewa ya baridi. Pia hutengeneza masweta kwa ajili ya watoto wa chekechea na wanafunzi wa Shule za Sekondari.

Uanachama

Shirika hili hupokea wasichana waliomaliza darasa la saba na kuendelea. Shirika vile vile linampango wa kuwaendeleza kielimu wanachama wake. Malezi yao ni kama ifuatavyo:

Aspiranti miaka miwili,

Postulanti mwaka mmoja,

Novisiati miaka miwili halafu nadhili za mwanzo.

Nadhili za Daima huweka miaka sita baada ya nadhili za mwanzo au za muda.


Sr. Leonia Mdoe
MIRADI MBALIMBALI

* Montessori Training Center – Ubiri - Lushoto, Tanga
* St. Eugene Hotel – Ubiri – Lushoto, Tanga
Hostel hii inasaidia uendeshaji wa Montessori Training Center.

Non-commercial Community Projects

* Forestation – Kwamndolwa Sisters Convent
- The benefits of this project are environmental preservation as well as wood for fuel and timber.
* Agriculture (farming and animal raising) – Kwamndolwa Sisters Convent
- We grow all sorts of cereal and vegetable crops, raise cattle, pigs, and chickens for community sustenance.
* Biogas – Kwamndolwa Sisters Convent

St. Eugene Hostel
- Biogas is a by-product from our livestock: we use it for fuel and light.
* Catechetical Training Center – Rangwi Sisters Convent
- Trains and prepares the sisters to evangelize
* St. Pius Homecraft Center – Rangwi Sisters Convent
- Trains and provides girls and young women with domestic skills, sewing, etc.
* Health Center – Kwamndolwa Sisters Convent
- Provides healthcare for the community and the neighboring families
* Montessori Nursery School - Kwamndolwa Sisters Convent
- Trains and provides little children with learning and social skills
* Water - Kwamndolwa Sisters Convent, Rangwi Sisters Convent
Montessori Teachers Training Center