PAROKIA YA MT. MAXIMILLIAN MARIA KOLBE
MKATA TANGA
DEKANIA YA HANDENI
Parokia ya Mt. Maximillian Maria Kolbe (2022) RATIBA YA IBADA: |
Mt. Maximillian Maria Kolbe Nyumba ya mapadre |
Ujenzi wa ofisi ya parokia | |
Uchimbaji kisima cha maji parokiani | |
Utanuzi wa kiwanja cha parokia | |
Uongozi wa parokia ya Mkata | |
Kisima cha maji ya mvua parokiani Mkata | |
Changamoto za utume vigangoni kipindi cha mvua | |
Watoto wakishiriki mafundisho ya dini | |
Watoto utoto wa Yesu walipotembelea uwanja wa ndege Tanga |
HISTORIA YA PAROKIA
Kutokana na ongezeko la Wakristo na ukuaji wa kasi wa kijiji cha Mkata, kutokana na uwekezaji wa serikali, na hasa ujenzi wa Halmashauri ya Handeni
vijijini, mnamo tarehe 30.04. 2022 aliyekuwa msimamizi wa Jimbo la Tanga na sasa Mhashamu Baba Askofu Thomas Kiangio, alitangaza Kigango cha
Mt. Anthony wa Padua kuwa Parokia tarajiwa, Padre James Elias Kabosa alitumwa kuwa Padre Mkazi wa Parokia tarajiwa, akiwa anaishi parokia ya Handeni
na kutoa huduma Parokia hii tarajiwa.
Katika ibada ya misa hija ya kijimbo huko Gare, yaani tarehe 14.10.2022, msimamizi wa Jimbo alitangaza Parokia tarajiwa ya Mkata kuwa Parokia kamili.
Parokia hii iliundwa kwa mara ya kwanza na vigango vya Mkata,(zamani Kigango cha Kabuku) Kwachaga (zamani kigango cha Handeni), Kitumbi zamani kigango cha
Kabuku)na Kwedihuo (zamani kigango cha Parokia tarajiwa Mkalamo), somo wa Parokia akiwa bado ni Mtakatifu Anthony wa Padua.
Mnamo tarehe 29.04.2024 tuliadhimisha rasmi ibada ya uzinduzi wa Parokia ya Mkata lakini pia kumtangaza rasmi somo na msimamizi wa Parokia na kuwa
Mt. Maximilian Maria Kolbe. Sababu ya msingi ya kubadilisha ni kuwepo tayari parokia ya Mt. Anthony wa Padua, kanisa kuu ambaye pia ni msimamizi wa
Jimbo letu la Tanga, pia kwa ajili ya kuunganisha undugu na Parokia rafiki ya huko Munich Ujerumani.
Kwa sasa Parokia ina vigango 8 na ilianza na waumini kati ya 83 hadi 120 hivi waliokuwa hai, na sasa Parokia nzima ina waumini 1499, kadiri ya sensa ya
kiparokia ya machi mwaka 2024.