PAROKIA YA BIKIRA MARIA MALKIA NA MAMA
HALE TANGA
DEKANIA YA KOROGWE


Parokia ya Bikira Maria malkia na Mama (1974)
S.L.P. 483, Hale, Korogwe, Tanga
Tanzania

RATIBA YA IBADA:
JUMAPILI:
Misa 1: saa 12:30 Asubuhi.
Misa 2: saa 02:30 Asubuhi.
Misa 3: saa 10:00 jioni (Misa ya watoto).

SIKU ZA JUMA;
Jumatatu hadi Jumamosi saa 12:30 Asubuhi

Mapadre:
Pd. Thomas Msagati: Paroko


Bikira Maria Malkia na Mama
somo wa Parokia.
Sherehe yake ni kila
Tarehe 22 Agosti


Nyumba ya mapadre

Screenshot

Kanisa la parokia


parokia_chumbageni_kikanisa cha kuabudu

Eneo la parokia

HISTORIA YA PAROKIA
Parokia ya Hale imejengwa kandokando katikati ya miji ya Muheza na Korogwe kandokando ya barabara kuu inayounganisha miji ya Tanga na Dar-Es-Salaam/Arusha. Parokia ya Hale ilianza kama kigango cha Parokia ya Potwe. Mapadre wa ki-Rosmini waliokuwa wakiishi Parokiani Potwe, walitoa huduma za kichungaji katika kigango hiki na vigango vingine katika eneo hili. Jengo la kwanza la ibada katika kigango hiki lilikuwa ndani ya kambi ya mkonge ya shamba la Hale kambi ya Makinyumbi hatua kadhaa magharibi ya Mto Pangani kandokando ya barabara kubwa inayounganisha miji ya Tanga na Korogwe. Sehemu kubwa ya waumini waliokuwa wakiabudu katika kigango hiki walikuwa ni waajiriwa wa shamba la mkonge la Hale ambao wengi wao walitokea mikoa ya bara. Waumini wachache walikuwa ni wenyeji wa sehemu hii.
Katika miaka ya mwanzoni mwa 1970, idadi ya wakazi wa kitongoji cha Makinyumbi na vitongoji jirani ilikuwa inaongezeka kwa haraka. Kijiji cha Hale kilianza kuwa na mvuto kwa wajasiliamali wadogowadogo na hivi kuanza kufungua maduka madogo madogo pembezoni mwa barabara kuu. Pia mradi wa mgodi wa umeme ulileta waajiriwa wengi toka sehemu mbalimbali nchini. Mpanuko huu wa watu katika maeneo haya uliongeza pia idadi ya waumini wa-Katoliki. Katika mwaka 1974, mheshimiwa padre John Haule (mmisionari kutoka jimbo la Songea) ambaye alikuwa akifanya utume jimboni Tanga, alitumwa kufanya utume Makinyumbi kama padre mkazi.
Jengo la kanisa la wakati huo lilikuwa ndani ya kambi ya mkonge ya Makinyumbi na lilikuwa limejengwa na menejimenti ya shamba hilo la mkonge kwa ajili ya huduma za kiroho za wafanyakazi wa-Katoliki. Kwa padre Haule kutumwa katika eneo hili, menejimenti ya shamba la mkonge la Hale ilitenga nyumba moja ya kambi kwa ajili matumizi yake. Tukio hili la padre kuishi kambini Makinyumbi lilikuwa ni vuguvugu la uanzishaji wa parokia ya Hale. Bahati mbaya kutokana na sababu za pekee, padre Haule aliondolewa Makinyumbi na kurudishwa kuishi Parokiani Potwe.
Katika miaka ya mwanzoni mwa 1980 sensa ya watu iliongezeka katika maeneo ya Makinyumbi na kulifanya kanisa la Makinyumbi kutokidhi mahitaji ya ongezeko hili. Katika mwaka 1982, mheshimiwa padre Francis Quinn, I.C. aliiomba menejimenti ya shamba la mkonge la Hale sehemu ya nchi ya kujenga parokia. Menejimenti ya shamba ilitoa sehemu kubwa ya shamba kwa lengo hilo upande wa kaskazini mwa barabara kuu ya Tanga-Korogwe. Katika mwaka huohuo, padre Quinn alianza kujenga nyumba ya masista na pia kujenga jengo kubwa la kanisa. Miaka miwili baadye katika mwaka 1984 jengo la kanisa lilikamilika na jengo hili lilibarikiwa na Mhashamu baba askofu Maurus Komba. Padre Quinn aliteulikwa kuwa paroko wa kwanza wa parokia hii. Pamoja na hayo padre Quinn alikaa muda mfupi katika parokia ya Hale na baadaye aliondoka. Mapadre wa ki-Rosmini waliikabidhi parokia hii kwa askofu wa jimbo na baba askofu alimtuma mheshimiwa padre Gerald Chilambo kuwa paroko wa kwanza mzalendo.
Japo nyumba ya masista ilikuwa ni ya kwanza kujengwa katika parokia hii, masista hawakufika katika parokia hii mpaka baadaye. Hivi kwa kuwa nyumba ya mapadre ilikuwa bado haijajengwa, mapadre wa mwanzo katika parokia hii waliitumia nyumba ya masista kama nyumba ya mapadre. Ilikuwa baadaye sana wakati wa uongozi wa mheshimiwa padre Titus Mdoe aliyesimamia ujengwaji wa nyumba ya mapadre. Ni katika muda wa uongozi wa mheshimiwa padre Ernest Seng’enge, masista wa COLU walifika parokiani Hale kuanza utume wao.

Mapadre wazawa wa Parokia ya Hale ni: Aloyce Babene, C.P. (2006), Peter Kagaba (2009), na James Kabosa (2011).