PAROKIA YA MCHUNGAJI MWEMA
KWALUKONGE TANGA
DEKANIA YA KOROGWE
Parokia ya Mchungaji Ma (2003) RATIBA YA IBADA: |
Yesu Mchungaji Mwema
|
|
HISTORIA YA PAROKIA
Parokia ya Kwalukonge imejengwa maili kadhaa kusini ya mji wa Mombo kandokando ya barabara ndogo ya mkato itokayo mji wa Mombo
kupitia shamba la ngombe la Mzeri kuelekea Handeni. Hapo awali Kwalukonge ilikuwa ni kigango cha Parokia ya Mazinde. Baadaye
kigango hiki kikawa sehemu ya Parokia ya Mombo. Kanisa la awali la kigango cha Kwalukonge lilikuwa ndani ya kambi ya shamba la
mkonge la Kwalukonge. Wakati huo Kwalukonge lilikuwa shamba dogo la mkonge lilikokuwa chini ya usimamizi wa shamba la mkonge mama
la Mazinde.
Idadi ya wakazi wa Kwalukonge iliongezeka sana baada ya mwaka 1967 wakati serikali ilipoanzisha kijiji cha ujamaa cha
Magamba-Kwalukonge. Watu wengi toka nchi ya Lushoto na sehemu nyinginezo walihamia kijijini Magamba-Kwalukonge kuweza kulima na
wengine kufuga. Kwa misaada toka serikalini na kutoka mashirika binafsi, wananchi wa kijiji hiki waliweza kupata misaada ya elimu
ya kilimo bora na hivi kuongeza umaarufu wa kijiji hiki katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara. Kilimo cha mazao ya
karanga na mahindi kilishamiri sana katika kijiji hiki na kuweza kulisha watu wengi wa makazi ya milima ya Usambara. Katika jumla
hii ya watu waliohamia hapo kijijini kulikuwa na idadi kubwa ya watu wa madhehebu ya ki-Katoliki. Hivi waumini wa ki-Katoliki
waliokuwa ni wafanyakazi wa shamba la mkonge waliungana na wale walioishi katika kijiji cha ujamaa na kuifanya jumuia hii kuwa
yenye nguvu sana.
Jinsi siku zilivyosogea mbele na namba ya waumini kuwa kubwa katika Kwalukonge, hitajiko la sehemu kubwa ya shughuli za kanisa
ilihitajika. Baba askofu alimtuma mheshimiwa padre Nazzareno Natale, I.C. kuweza kujenga parokia ya Kwalukonge. Padre Nazzareno
aliweza kufika Kwalukonge na kuweza kupata sehemu kubwa ya nchi toka shamba la mkonge la Kwalukonge kujenga parokia. Baada ya
kupata eneo hili padre Nazzareno alijenga kanisa kubwa la kudumu katika eneo hilo na pia alijenga nyumba ya mapadre na nyumba
ya masista pamoja na shule ya chekechea. Hatimaye padre Nazzareno aliweza kujenga shule ya sekondari ambayo aliikabidhi kwenye
uongozi wa serikali kwa uendeshaji wake.
Baada ya ujenzi wa parokia hii, baba askofu alilitabaruku kanisa hili na kukiinua kigango cha Kwalukonge kuwa parokia
inayojitegemea. Baada ya kukamilisha ujenzi wa parokia hii, padre Nazzareno aliondoka. Hadi hivi sasa mapadre wa ki-Rosmini
wanaendelea kutoa za kichungaji parokiani hapa wakishirikiana na timu ya masista wa shirika la Mama Yetu wa Usambara (COLU).
Historia ya seminari ndogo ya Soni inaonyesha kwamba kulikuwa na vijana wengi waliosoma hapo seminarini wakitokea maeneo ya
Kwalukonge lakini hakuna aliyeweza kusogea mbele na kulijongelea daraja la upadre hadi hivi leo.