PAROKIA YA MT. YOSEFU MUME WA BIKIRA MARIA
MOMBO TANGA
DEKANIA YA KOROGWE
Parokia ya Mt. Yosefu mume wa Bikira Maria (1986) RATIBA YA IBADA: |
Mt. Yosefu mume wa Bikira Maria Nyumba ya Mapadre |
|
HISTORIA YA PAROKIA
Parokia ya Mombo ipo chini ya milima ya Usambara. Parokia hii ipo katika njia panda. Barabara kuu ya Korogwe – Moshi inakutana
hapa na barabara ya Mtae/Lushoto-Mombo.
Kwa asili yake Mombo ilikuwa ni kigango cha parokia ya Mazinde. Katika miaka ya awali ya 1960 jengo dogo la kanisa lilijengwa hapa
kuhudumia jumuia ndogo ya wa-Kristu iliyokuwa ikiishi Mombo. Sehemu kubwa ya waamini hawa walikuwa wakifanya kazi kwenye kampuni ya
reli na pia kwenye shamba la mkonge la Mombo na mashamba mengine ya mkonge ya jirani kama vile Mwelya. Baadhi yao walifanya kazi
katika kiwanda cha mbao cha Sandali-Mombo.
Katika miaka ya mwanzoni mwa 1970, mji Mombo ulipanuka kibiashara na kimakazi. Biashara nyingi ndogondogo zilifunguliwa na hivi
kuvutia watu wengi. Ongezeko hili la watu lilishinikiza mabadiliko katika mtazamo wa kichungaji. Mheshimiwa padre Donal Sullivan,
I.C. na bruda Jim Mariot, I.C. walianza upanuzi wa lililokuwa jengo la kanisa la Mombo. Baadaye chini ya uongozi wa mheshimiwa
padre Anthony Mitchell, I.C. nyumba ya masista na shule ya chekechea zilijengwa parokiani hapo.
Katika mwaka 1986 baba askofu alikitangaza kigango cha Mombo kuwa parokia inayojitegemea ikiwa ina vigango vyake vilivyopanuka
tokea Kwalukonge hadi sehemu za Kwasunga.
Padre mzawa wa Parokia ya Mombo ni: Andreas Shekuamba (2000).