PAROKIA YA MT. PATRICK
KONGOI TANGA
DEKANIA YA LUSHOTO
Parokia ya Mt. Patrick (1966) RATIBA YA IBADA: |
Mt. Patrick Kituo cha afya parokiani Kongoi |
Parokiani Kongoi |
HISTORIA YA PAROKIA
Kitongoji wa Nkongoi kipo katikati ya milimi ya Usambara magharibi umbali wa kilometa 52 mashariki ya mji wa Lushoto. Hapo zamani Nkongoi ilikuwa
ni moja ya vigango cha Parokia ya Gare. Mapadre toka parokiani Gare walitembea kwa miguu kwenda kutoa huduma za kichungaji katika nchi ya Nkongoi
na majirani zake. Kwa kuwa mwendo ulikuwa ni mrefu tokea Gare, mapadre hawa walipiga kambi Nkongoi kwa siku kadhaa wakitoa huduma za kiroho hapo
Nkongoi na vijiji vya jirani. Katika mwaka 1965 mheshimiwa padre Yosefu Stout, I.C. alitumwa Kongoi kutokea Gare ili anzishe rasmi Parokia ya Nkongoi.
Padre Stout alifuatiwa na mheshimiwa padre Tom Burke, I.C. na sista Clarice, OSB waliotokea USA. Sista Clarice alikuwa ni tabibu wa afya za watu.
Baadaye padre Tom Burke na sista Clarice walirudi USA na kumuacha padre Yosefu Stout peke yake kule Nkongoi.
Mapadre hawa wa mwanzo katika nchi ya Nongoi walishiirikiana kwa karibu na makatekista wa maeneo haya. Mmoja wa makatekista wa awali katika eneo hili
alikuwa ni bwana Ernesti Abdala ambaye ni mwenyeji wa kijiji cha Yamba. Bwana Ernesti Abdala bado yu hai hivi sasa (2013) akiwa na miaka 91, alifanya
kazi kubwa ya kufundisha dini kwa wana-Nkongoi. Bwana Ernesti Abdala amekuwa ni uti wa mgongo wa enezo la imani Katoliki katika nchi hii ya Nkongoi
Mara moja Mhashamu Baba Askofu Arthurs, I.C. pamoja na mheshimiwa padre Kennedy, I.C. walitembelea Nkongoi kwa shughuli za kichungaji. Walipokuwa
wakiadhimisha ibada ya misa takatifu walimwona mtoto mmoja tu aliyehudhuria ibada hiyo. Hii iliwaogopesha wageni hawa. Mara moja baba askofu alitoa
maelekezo kwa paroko wa wakati huo kwamba inapaswa kuanza ujenzi wa shule ya msingi parokiani hapo. Baba askofu alifahamu kwamba uwepo wa shule ya
msingi katika mazingira ya hapo parokiani ungevuta watoto wengi katika masomo na maarifa ya kidunia lakini pia ingekuwa ni nafasi njema ya kuwalea
watoto hao katika maisha yao ya kiroho. Basi ujenzi wa shule ya msingi ulianza mara moja. Shule hiyo imekuwa ni zawadi kubwa kwa wana-Nkongoi.
Ujenzi wa kanisa kubwa na la kudumu ulifanyika baadaye sana katika kipindi cha uongozi wa mheshimiwa padre Francis Quinn, I.C. na baadaye kuweza
kukamika wakati wa uongozi wa mheshimiwa padre Edmund Spillane, I.C. Pamoja na ujenzi wa kanisa la parokia, ufadhili ulipatikana wa kuweza kujenga
zahanati ya afya kwa ajili ya huduma za afya ya akina mama na watoto katika maeneo haya. Zahanati hii imekuwa ni mkombozi mkubwa kanisa eneo hili
kwa kuweza kutoa huduma ya kwanza kwa wagonjwa wa maeneo haya kabla hawajafikiriwa kupelekwa hospitali za Bumbuli au Lushoto kwa kesi kubwa.
Utume wa Injili katika nchi ya Nkongoi uliboreka zaidi kwa kutumwa kwa masista wetu wa shirika la masista wa Mama Yetu wa Usambara kutoa huduma za
kichungaji katika parokia hii. Masista wetu hapo parokiani wanafanya utume wa kufundisha dini, kufunza shule ya msingi, na pia kutoa huduma katika
zahanati ya Nkongoi.
Katika mwaka 1988, uongozi wa shirika la mapadre wa-Rosmini waliikabidhi parokia ya Nkongoi jimboni na hapo baba askofu alimtuma mheshimiwa padre
Francis Gembe kuwa paroko na padre mkazi mzalendo wa kwanza katika historia ya parokia. Wakati huohuo mheshimiwa padre Peter Rodoussakis alipelekwa
parokiani hapo kuwa padre msaidizi.
Mapadre wazawa wa parokia ya Nkongoi ni: Msgr Dennis Mavunga (1975),
Msgr Stanislaus Baruti (1989) (R.I.P.), Patrick Mngano (2003) (R.I.P.),
Cornelius Mdoe, O.S.B. (2004) (R.I.P.).