PAROKIA YA MT. FRANCIS XAVIER
KWAI TANGA
DEKANIA YA LUSHOTO


Parokia ya Mt. Francis Xavier (1965)
S.L.P 54, kwai, Tanga
Tanzania

RATIBA YA IBADA:
JUMAPILI:
Misa: saa 04:30 Asubuhi.

SIKU ZA JUMA;
Jumatatu hadi Jumamosi saa 12:30 Asubuhi

Mapadre:
Pd. Passian Kika: Paroko


Mt. Francis Xavier
somo wa Parokia.
Sherehe yake ni kila
Tarehe 03 Desemba


Kituo cha Afya Kwai

Eneo la Kituo cha Afya


Majengo ya zamani chuo cha ukatekista Kwai

HISTORIA YA PAROKIA
Parokia ya Kwai ipo katikati ya milima ya Usambara magharibi kandokando ya barabara ndogo inayounganisha mji wa Lushoto na vijiji vya Mlola, Malibwi, na Kwekanga. Hapo zamani, Kwai ilikuwa ni kigango cha Parokia ya Gare. Katika mwaka 1965 uongozi wa jimbo ulikitangaza kingango hiki kuwa parokia inayojitegemea. Katika miaka ya mwishoni mwa 1960, jimbo lilijenga chuo cha makatekista. Wanafunzi wa chuo hiki cha makatekista walifika kuchukua masomo ya ukatekesta katika chuo hiki wakiwa na familia zao. Kwa bahati mbaya chuo hiki kilisitisha kutoa masomo hayo kutokana na ubovu wa majengo yake ambayo yalionyesha nyufa nyingi na hivi kuwa hatari kwa wanafunzi na familia zao.
Ubovu wa majengo ya chuo na parokia yaliusukuma uongozi wa mheshimiwa padre Sean Madden, I.C. katika miaka ya mwishoni mwa 1970 kuanza kujenga majengo mapya ya parokia kwenye kiwanja bora zaidi hapo parokiani. Padre Madde aliweza kujenga kanisa jipya na kubwa, nyumba nzuri ya mapadre, nyumba nzuri ya masista na pia zahanati ambayo hivi sasa imepata hadhi ya kuwa kituo cha afya.
Mheshimiwa padre Madden anakumbukwa sana katika uinjilishaji wa parokia ya Kwai haswa katika mwelekeo wake wa kupanda imani ya ki-Kristu kwa wananchi wa kabila la wa-Mbugu. Kabila hili ni kabila dogo ambalo linaishi katikati ya makabili ya ki-Pare na ki-Sambaa. Padre Charles Mhina (R.I.P) ni padre wa kwanza kupadirishwa jimboni Tanga akitokea kwenye kabila hili la ki-Mbugu.
Baada ya padre Madden kuondoka parokiani hapo, shirika la ki-Rosmini lilimtuma mheshimwa padre Edmund Spillane, I.C, kuwa paroko wa Kwai. Katika uongozi wa padre Spillane, miradi mingi ya uboreshaji wa parokia ilifanyika na kuipendezesha parokia hii.
Hadi hivi sasa parokia hii inahudumiwa na mapadre wa shirika la Mapendo. Pamoja nao ni uwepo wa masista wetu wa COLU ambao uchungaji wao ndani ya parokia unaendelea kuipanda roho ya Injili kwa wana-Kwai. Uinjilishaji katika Kwai umejitokeza sana katika kuwa na miito mingi ya kitawa kwa wasichana toka parokia hii ambao wengi wamejiunga na shirika la masista wa COLU.

Padre mzawa wa Parokia ya Kwai ni: Charles Mhina (1987) (R.I.P.).