PAROKIA YA MT. BENEDIKTO
MABUGHAI TANGA
DEKANIA YA LUSHOTO
Parokia ya Mt. Benedikto (2010) RATIBA YA IBADA: |
Mt. Benedikto wa Nursia
|
|
HISTORIA YA PAROKIA
Parokia ya Mabughai imo ndani ya milima ya Usambara umbali wa kilometa 12 hivi kutoka mjini Lushoto. Parokia hii ndani ya kijiji cha Mabughai.
Kijiji cha Mabughai kimejengwa kandokando ya barabara inayounganisha miji ya Lushoto na Mlalo au Mtae.
Hapo awali Mabughai ilikuwa ni moja ya vigango vya Parokia ya Lushoto. Mapadre toka parokiani Lushoto walifika hapo kigangoni kila Jumapili kwa
madhehebu ya misa na masakramenti ya kanisa. Waumini wengi wa Mabughai wamekuwa ni wananchi wenyeji wa mazingira haya lakini pia waajiriwa wengi
katika taasisi zilizonguka kigango hiki. Taasisi hizo zilikuwa chuo cha maendeleo ya akina mama Mazinde Juu
(hivi sasa sekondari ya wasichana Mazinde Juu), chuo cha maendeleo ya wananchi Mabughai, sekondari ya wavulana ya Magamba (ambayo sasa ni chuo kikuu
cha Askofu Sebastian Kolowa), chuo cha ufundi cha Magamba na viwanda vya mbao vilivyozunguka maeneo ya kijiji cha Magamba.
Mara kadha wa kadha mapadre wa Shirika la Roho Mtakatifu wenye nyumba yao ya wanovisi katika kijiji cha Magamba waliweza kushirikiana kiuchungaji
katika kigango hiki. Pia mheshimiwa padre Damian Milliken, O.S.B. ambaye alikuwa akifundisha shule ya sekondari ya Magamba katika miaka ya mwishoni
mwa 1970 na mwanzoni mwa 1980 aliweza kushiriki katika shughuli za kichungaji katika kigango hiki.
Katika miaka ya mwisho ya 1980 padre Damiani alipata ruhusu toka jimboni kuweza kuanzisha shule ya ya sekondari ya Mazinde Juu ambayo iliweza
kufunguliwa rasmi mwaka 1989. Shughuli za uboreshaji na ujenzi wa sekondari ya Mazinde Juu umeenda sambamba na shughuli za uboreshaji wa jingo
la kanisa la kigango cha Mabughai. Kutojana na ujirani wa shule ya sekondari ya Mazinde Juu na kigango cha Mabughai, ushirikano wa karibu wa
taasisi hizo mbili ulijengeka. Siku zilivyozidi kusonga mbele idadi ya waumini ilizidi kuongezeka katika maeneo ya kijiji cha Mabughai na vijiji
vya ujirani. Kutokana na ongezeko hilo jengo la asili la kanisa la kigango halikuweza kutosha kwa idadi ya waumini waliopo. Kwa ushirikiano wa
waumini wa Mabughai na wafadhili toka nje, padre Damiani aliweza kufanikiwa kujenga jengo kubwa la kanisa hapo Mabughai.
Baada ya kutabarukiwa jengo hili jipya la kanisa la Mabughai, mhashamu baba askofu Anthony Banzi wa Jimbo la Tanga alikiinua kigango cha Mabughai
kuwa Parokia ya Mabughai na kumteua mheshimiwa padre Damian Milliken, O.S.B. kuwa paroko mwasisi wa parokia.
Upendo na nia ya padre Damiani kwa ubora na maendeleo ya kielimu kwa wananchi wa Mabughai na majirani zake ni mkubwa mno. Moja ya mradi mkubwa
ambao ameuanzisha parokiani ni shule ya Mtakatifu Benedikto ya ki-Ingereza. Shule hii inawasaidia vijana wa maeneo haya kuwa na uwezo wa lugha
ya ki-Ingereza, hesabu, na sayansi kama sehemu ya maandalizi yao kuweza kujiunga na shule bora za sekondari nchini na pia elimu hiyo kuwasaidia
kuendelea vyema katika masomo yao hayo katika shule za sekondari na katika elimu ya juu. Kutokana na maandalizi haba ya vijana hawa, mara nyingi
huko nyuma wameshindwa kupata nafasi za masomo katika shule bora nchini. Shule hii imekuwa mkombozi mkubwa kwa watoto na familia za maeneo haya.
Padre Damiani anaendelea kuiboresha Parokia ya Mabughai. Hivi sasa yumo katika harakati za kujenga nyumba ya mapadre na pia nyumba ya masista.
Ni lengo lake kwamba baada ya kukamilisha mradi huu, basi mapadre na masista waishi hapa parokiani katika kazi ya uinjilishaji wa wana Mabughai.
Padre mzawa toka katika Parokia hii ya Mabughai ni: Augustino Mahonge (2009) ambaye ni padre wa Jimbo Kuu la Chikago, USA.