PAROKIA YA MT. THERESIA WA MTOTO YESU
MALINDI TANGA
DEKANIA YA LUSHOTO


Parokia ya Mt. Theresia wa Mtoto Yesu (1976)
S.L.P. 42, Malindi, Lushoto, Tanga
Tanzania

RATIBA YA IBADA:
JUMAPILI:
Misa 1: saa 02:00 Asubuhi.
Misa 2: saa 09:00 Mchana (Misa ya watoto).

SIKU ZA JUMA;
Jumatatu hadi Jumamosi saa 12:30 Asubuhi

Mapadre:
Pd. Maximillian Mahonge: Paroko


Mt. Theresia wa Mtoto Yesu
somo wa Parokia.
Sherehe yake ni kila
Tarehe 01 Oktoba


Ndani ya kanisa la Malindi

Kanisa la zamani Malindi

HISTORIA YA PAROKIA
Parokia ya Malindi ipo ndani ya milima ya Usambara magharibi kilometa kama 20 tokea mji wa Lushoto. Parokia hii imejengwa kwenye njia ya panda inayounganisha mji wa Lushoto na miji ya Mtae na Mlalo. Inasemekana kwamba hapo awali Malindi ilikuwa ni kigango cha Parokia ya Kwai. Pamoja na hayo wengine wanasema kilikuwa kigango cha parokia ya Gare. Inazungumzwa kwamba mheshimwa padre Francis Hubsch, I.C. aliweza kujenga kikanisa kidogo katika nchi ya Malindi katika mwaka 1937 kwa ajili ya jumuia ya matumizi ya ibada kwa wa-Katoliki katika maeneo hayo. Inawezekana kwamba padre Hubsch alifika katika nchi ya Malindi akitokea Gare kupitia Kwai. Hata hivyo baada ya masista wa shirika la Mama Yetu wa Usambara kufungua makao yako makuu Rangwi, mapadre walezi wa masista hao walikwenda kutoa huduma ya kichungaji katika kanisa la Malindi na vitongoji jirani. Baadaye baada ya Rangwi kuundwa kuwa parokia, Malindi ikawa ni kigango cha Rangwi.
Katika mwaka wa 1972 Malindi ilifanywa kuwa parokia inayojitegemea. Pamoja na uundwaji wa parokia hiyo, bado waumini alikuwa wakitumia kikanisa kilichojengwa mwaka wa 1937. Mapadre waliohudumia parokia hiyo bado waliendelea kuishi parokiani Rangwi.
Jumuia ya ki-Katoliki katka Malindi iliendelea kukua sana katika miaka ya 1980 hata kulifanya jengo la kanisa la Malindi kuwa dogo mno. Katika mwaka 1988, mapadre wa ki-Rosmini waliirudisha parokia ya Malindi kwa askofu. Katika mwaka huo baba askofu alimteua mheshimiwa padre Joseph Mbenna kuwa paroko na padre wa kwanza mzalendo kuiongoza parokia ya Malindi. Kwa kushirikiana na mheshimiwa padre Athanas Meixner, O.S.B paroko wa Parokia ya Soni, padre Mbenna na waumini wa Malindi waliweza kujenga kanisa kubwa la kisasa ambalo lilitabarukiwa na Mhashamu Askofu Telesphor Mkude katika mwaka 1993. Baada ya ujenzi wa kanisa, padre Mbenna aliweza kujenga nyumba ya mapadre na kuweza kuhamia kuishi hapo
Parokia ya Malindi ina vigango 11. Baadhi ya vigango hivi vina majengo ya makanisa yao lakini vingine havina na hivi vinalazimika kuazima madarasa ya shule kuweza kuendeshea ibada.

Padre mzawa kutoka Parokia ya Malindi ni: Maurus Shemdoe (2003) (R.I.P.).