PAROKIA YA MT. BENEDIKTO
TEKWA TANGA
DEKANIA YA LUSHOTO
Parokia ya Mt. Benedikto wa Nursia (2001) RATIBA YA IBADA: |
Mt. Benedikto wa Nursia Ndani ya kanisa |
Waamini wakishiriki ibada ya Jumapili parokiani Tekwa
| Altare katika kanisa la Tekwa
| Nyumba ya mapadre parokiani Tekwa |
HISTORIA YA PAROKIA
Parokia ya Tekwa imo katikati ya milima ya Usambara ya kati. Awali Tekwa ilikuwa ni kigango cha Parokia ya Sakharani. Maeneo mengi yanayozunguka
Parokia hii ni mashamba ya wananchi ya chai na umbali mchache toka parokiani ni kiwanda kikubwa cha kutengenezea chai cha Mponde. Kuifikia parokia
hii unaweza kutumia barabara ndogo za kutokea miji ya Soni kwenda Bumbuli kupitia kiwanda cha chai cha Mponde. Njia nyingine ile ya kutokea Korogwe
kupitia Kwashemshi na Dindira hadi Mponde.
Ongezeko la idadi ya wa-Katoliki katika maeneo ya Tekwa, yalimsukuma aliyekuwa paroko wa wa Parokia ya Sakharani mheshimiwa
padre Burkard Schneider, OSB ajenge makao makuu ya kigango hiki katika ngazi ya kiparokia. Hivi aliweza kujenga kanisa kubwa,
nyumba ya mapadre, nyumba ya masista, na shule ya chekechea katika eneo hili. Pia alitengeneza muundo wa kukinga maji toka mapaa ya
majengo haya kwa matumizi ya wakazi wa hapa. Baada ya kukamilisha majengo haya, padre Burkard alimkabidhi baba askofu kituo hiki.
Kanisa la kigango hiki lilitabarukiwa katika mwama 2001 na kuwekwa chini ya ulinzi wa Mtakatifu Benedikto wa Nursua. Ni katika mwaka
huo huo baba askofu aliitangaza Tekwa kuwa parokia inayojitegemea na kumtuma mheshimiwa padre Joseph Sikija kuwa paroko mzalendo wa
kwanza kuiongoza parokia hiyo.