PAROKIA YA BIKIRA MARIA MALKIA WA AMANI
AMANI TANGA
DEKANIA TANGA MJINI
Parokia ya Bikira Maria malkia wa Amani (1985) RATIBA YA IBADA: |
Bikira Maria Malkia wa amani Nyumba ya Watawa |
Eneo la Parokia ya Amani | |
Kanisa la Amani |
a). Mahali Ilipo Parokia
Parokia ya Amani ipo katika milima ya Usambara mashariki. Parokia hii imejengwa katikati ya mashamba ya zao la chai. Ipo barabara moja ndogo ambayo ni kiungo
kikubwa cha barabara zitokazo mashamba ya chai na vijiji vya wananchi kwenda Bombani na hatimaye kuufikia mji wa Muheza.
b). Chimbuko la Parokia
Hapo awali parokia ya Amani ilianza kama kigango cha parokia ya Muheza. Parokia hii ilianzishwa na mheshimiwa padre Jackie Reid, I.C. aliyekuwa paroko wa parokia
ya Muheza. Katika miaka ya 1970, padre Reid alianza parokia hii kwa kujenga jengo la kanisa. Ujenzi wa kanisa ulikamilika mwaka 1985.Baba Askofu Maurus Komba
alilibariki jengo hili la Kanisa Mei 27, 1985. Padre Reid baadaye aliendelea kujenga nyumba ya mapadre na hatimaye nyumba ya masista.
c). Wakazi wa Amani
Wenyeji halisi wa maeneo ya Amani ni wa-Sambaa. Pamoja na hivi bado kuna watu wengi wa bara ambao walifika katika nchi ya Amani kufanya kazi katika mashamba ya
chai, na wengine wataalamu kufanya kazi katika kituo cha utafiti wa ugonjwa wa malaria na wengine katika taasisi za elimu. Wenyeji wengi wamezamia katika ukulima
wa viungo vya chakula na mazao mengine ya chakula na biashara.
d). Kipindi cha Mpito
Katika mwaka 1996,wamisionari waki-Rosmini ambao ndio waliofanya uinjilishaji katika parokia hii tangu mwanzo wake, waliikabidhi parokia hii kwa askofu wa jimbo
ambaye alimtuma mheshimiwa padre Stanistalaus Baruti (R.I.P) kuwa paroko wa kwanza mzalendo.
e). Maendeleo katika Parokia
Tokea siku za mwanzo wa utume wake pale Amani, mheshimiwa padre Baruti (R.I.P) alikuwa mvumbuzi mkubwa wa kuboresha uchungaji katika eneo hili. Padre Baruti alifungua
kituo kikubwa na kizuri cha maisha ya kiroho ambacho kinaendelea kuwaalika wakazi mahalia na wageni kuweza kupata utulivu mzuri wa maisha ya kiroho.
f). Utume wa Masista wa COLU
Parokiani Amani wapo masista wa shirika la Mama Yetu wa Usambara (COLU) ambao wanatoa huduma za kichungaji wakishirikiana na padre. Uwepo wao parokiani hapo ni
chachu kubwa ya Injili.