PAROKIA YA MT. JEMSI MKUU
MISOZWE TANGA
DEKANIA TANGA MJINI



Parokia ya Mt. Jemsi mkuu (2011)
S.L.P 180, Muheza,
Tanga, Tanzania.

RATIBA YA IBADA:
JUMAPILI:
Misa: saa 2:00 Asubuhi.

SIKU ZA JUMA;
Jumatatu hadi Jumamosi saa 12:30 Alfajiri

Mapadre:
Pd. Antoni Saguti: paroko


Mtakatifu Jemsi Mkuu
somo wa Parokia.
Sherehe yake ni kila
Tarehe 25 Julai


Jiwe la msingi la
Kanisa la Misowe

Kibao kioneshacho kanisa la Misozwe

Nyuma ya kanisa

HISTORIA YA PAROKIA
Parokia ya Misozwe ipo katika kata ya Misozwe kilometa kadhaa kaskazini ya mji wa Muheza chini ya milima ya Usambara mashariki. Hapo awali parokia hii ilikuwa ni kigango cha Parokia ya Mlingano. Katika miaka ya mwishoni mwa 1980, bwana Herbert Mtangi alitoa kilichokuwa kiwanja cha baba yake mzazi mzee James Mtangi ili kanisa lijengwe kwa heshima ya mzee huyu kwa ajili ya matumizi ya wa-Kristu wa maeneo hayo. Kwa ushirikiano wa karibu na uongozi wa mapadre wa Parokia ya Mlingano waheshimiwa Samuel Itatiro (R.I.P) na baadaye Bernard Chisi (R.I.P), waumini wa Misozwe wakiongozwa na bwana Herbert Mtangi walijenga jengo zuri la kanisa. Baada ya kukamilika kwa ujenzi huu wa kanisa, mhashamu baba askofu Anthony Banzi (R.I.P) alifika hapo kulibariki. Katika mwezi Mei 2002, baba askofu alimtuma mheshimiwa padre Anthony Mbenna kuwa mwangalizi wa parokia hii tarajiwa akiwa akiishi parokiani Mlingano. Baadaye padre Mbena aliweza kuhamia Misozwe ambako aliweza kupata ufadhili wa kuishi ndani ya nyumba ya bwana Herbet Mtangi hapo kijijini.
Wakati padre Mbena akiwa anaishi kwa bwana Mtangi, alikuwa akifanya juhudi ya kuandaa ujenzi wa nyumba ya mapadre hapo Misozwe. Padre Mbena hakuweza kuanza ujenzi wa nyumba ya mapadre hadi alipoondoka Misozwe Aprili 2006 lakini aliweza kuacha vifaa vingi vya ujenzi wa nyumba hiyo. Baada ya padre Mbena kuondoka Misozwe, parokia tarajiwa ilirudi tena kuwa kigango cha Mlingano.
Katika mwaka 2011 baba askofu banzi alimtuma mheshimiwa padre Emmanuel Mavengero kwenda Misozwe kama padre mkazi wa parokia tarajiwa. Katika mwaka huohuo baba askofu Banzi alimtuma mheshimiwa padre Ernest Seng’enge Misozwe kuwa padre msaidizi. Ni katika kipindi cha uongozi wa padre Mavengero basi nyumba ya kuishi mapadre ilikamilika kujengwa na kufanya Parokia.