PAROKIA YA BIKIRA MARIA NYOTA YA BAHARI
PANGANI TANGA
DEKANIA TANGA MJINI


A generic square placeholder image with a white border around it, making it resemble a photograph taken with an old instant camera


Parokia ya Bikira Maria Nyota ya Bahari (1973)
S.L.P 85, Pangani,
Tanga, Tanzania.

RATIBA YA IBADA:
JUMAPILI:
Misa: saa 01:00 Asubuhi.

SIKU ZA JUMA;
Jumatatu hadi Jumamosi saa 12:15 Alfajiri

Mapadre:
Pd. George Mhuza: Paroko

parokia_chumbageni_mtanthoni_wa_padua

Bikira Maria Nyota ya Bahari
somo wa Parokia.
Sherehe yake ni kila
Tarehe 10 Oktoba

parokia_chumbageni4

Eneo la kanisa

Screenshot

Mbele ya gani ni nyumba ya masista

HISTORIA YA PAROKIA
Pangani ilikuwa moja ya vigango vya Parokia ya Mtakatifu Teresia iliyo jijini Tanga. Vigango vingi vya Parokia ya Mtakatifu Teresia vilikuwa kusini mwa mto na mji wa Pangani. Hali hii ilifanya ugumu wa kuvifikia vigango hivyo kutokana na hali duni ya kivuko cha mto Pangani. Pantoni ya kuvusha magari na watu katika mto huu wa Pangani ilikuwa ndogo na chakavu na hivi ilizorotesha ubora wa kuvusha watu na magari katika kivuko hicho. Kutokana na uduni huu wa kivuko, ilikuwa ni kazi ngumu kwa mapadre toka parokiani Tanga kuvifikia vigango vilivyo kusini ya mto Pangani. Hali hii ilisukuma uanzishwa wa parokia ya Pangani. Ilionekana kwamba kukiwa na parokia katika mji wa Pangani pamoja na kwamba hapakuwa na waumini wengi katika mji huu wenye u-Isilamu mzito, ingesaidia mapadre waishio hapa kuweza kupanga utaratibu wa kuvuka kivuko na kuhudumia vigango kusini mwa mto.
Tokea mwaka 1973 mapadre walioishi Pangani walikuwa na utume mkubwa wa kuhudumia waumini wengi katika vigango vilivyojengwa ndani ya makambi ya mashamba ya mkonge yaliyotawanyika kaskasini na kusini mwa mto Pangani.
Mheshimiwa padre Francis Quinn, I.C. katika miaka ya themanini kati, aliweza kupata eneo kubwa la kujenga parokia ya Pangani. Kwa kusaidiana na mheshimiwa padre John Fortune, I.C waliweza kujenga kanisa kubwa, nyumba ya mapadre na nyumba ya masista. Kanisa lilikamilika na katika mwezi Machi 1989 na mhashamu baba askofu Telesphor Mkude alilibariki kanisa hili na kuliweka chini ya ulinzi wa Bikira Maria Nyota ya Bahari Baadaya ya kanisa kubarikiwa, mapadre wamisionari wa ki-Rosmini waliikabidhi parokia hii kwa baba askofu ambaye alimteua mheshimiwa padre Peter Rodoussakis kuwa paroko wa kwanza mwanajimbo kuiongoza parokia hii.
Hadi hivi sasa yapo mashirika mawili ya kidini ambayo yamefika Pangani kuanzisha miradi ya kiuchumi kwa ajili ya mahitaji ya jumuia zao. Mashirika haya ni Wafranskani/Makapuchini na masista wa kazi za Roho Mtakatifu toka Kilimanjaro. Uwepo wa watawa hawa ni mchango mkubwa wa uinjilishaji kwa wenyeji na wageni wa eneo hili la Pangani.