CATHOLIC DIOCESE OF TANGA

view this page in english

Communication Offices

 

Idara ya Habari ni nyenzo muhimu kurahisisha mawasiliano ndani ya Jimbo na nje ya Jombo. Mwanzoni ofisi ya habari ilitoa jarida la habari kila baada ya miezi mitatu. Hata hivyo, jarida hilo halikuendelea. Katika Jubilei ya miaka 100 ya Ukristo Jimboni Tanga, idara ilitoa Kitabu “HISTORIA YA JIMBO KATOLIKI TANGA 1893-1998”. Idara pia imefanikiwa kuweka habari muhimu kwenye tovuti “(www.tangadiocese.org)”. Idara pia imefanikiwa kuanzisha Redio ya Jimbo, “Redio Huruma F. M”. Lipo wazo la kuanzisha Runinga ya Jimbo kwa siku za usoni.

Shukrani kwa Padre Richard Kimbwi kwa kuimarisha mawasiliano Jimboni na nje ya Jimbo. Tutawakumbuka daima Wafanyakazi wetu wa mwanzo wa Redio huruma. Hawa ni Frenk Odomali, Lilyan Lihame, Joyce Kimwemwe, Daudi Lihunga, Janeti Sendega, Veronika Mtangi, Mwajisu Mwanamboka, Richard Valentino, Blandina George na Azaria Mwimbe. Pia mchango wa Shemasi Kihiyo Jandu, ambaye kwa sasa ni Padre na Paroko wa parokia ya Malindi hautasahaulika. Yeye alizipitia upya habari zilizopo kwenye tovuti na kuzihakiki, na ndie aliyesaidia kuleta tena tafsi ya Tovuti yetu toka lugha ya kiingereza kuja ya kiswahili. Na pia tafsri hiyo ndiyo imetumika katika kuandaa kitabu cha Jubilei ya miaka 50 tangu Tanga kuwa Jimbo.