KANISA KATOLIKI TANGA

view this page in english

UTUME WA WALEI

 

Kazi kubwa ya idara ni:

Kusaidia malezi ya Waamini Walei wakisaidiana na Makleri, kama ilivyonyambulishwa katika Mtakuso wa Pili wa Vatikan, kuishi muelekeo wa kijamii wa injili kiasi kwamba, ushuhuda huu unakuwa ni chachu ya chochote kinchofunga kukweli wa mtu.

Kushiriki katika kuwakomaza Waamini Walei kwa mafundinsho na tunu za Yesu kama zilivyoelezwa katika asasi mbalimbali za Kikristo chini ya mwamvuli wa barala la Waumini Walei; yaani WAWATA, UVIKATA, Moyo Mtakatifu wa Yesu, Wanaume Katoliki wa Tanzania (ONUM OMNES), Legia ya Maria, Mama wa Shauri Jema na vyama vingine vya Kitume.

Kuamsha umakini wa Waamini Walei katika kazi zao katika kushiriki maisha ya Kanisa la Yesu, Kanisa Moja, Takatifu Katoliki la Mitume kama umoja, chini ya mwongozo wa Waamini Walei ili kuleta majumuisho ambayo ni ya haki na upendo ndani ya jamii.

Kuwezesha na kuimarisha uzani kati ya maisha ya kila siku wa Waamini Walei na kujiota has kulinda heshima ya mtu katika masuala ya kijamii na kiuchumi.

Mkurugenzi wa utume huu Jimboni ni Mr. Slyvester Mgoma.