19 Machi, Sikukuu ya Mt. Yosefu Mume wa Bikira Maria

Sikukuu ya somo wa Seminary ya Soni na siku ya Wazazi

Jengo la maktaba na madarasa 4
Askofu A. Banzi, siku ya Mt. Yosefu Soni
Ujenzi wa dispensary Soni Seminary

19 March,

Ni sikukuu ya Mtakatifu Yosefu Mume wa Bikira Maria.

Mtakatifu Yosefu pia ni Somo wa Seminary ndogo ya Soni, katika Jimbo katoliki la Tanga. Mwaka huu wa 2007 siku hii imepewa rasmi jukumu maalumu na kuitwa siku ya wazazi.

Mwaka huu wa 2007 siku hii ilisherehekewa siku ya Jumamosi ya Tar. 17 Machi. Ilikuwa ni siku ya furaha kubwa sana kwa wazazi, wanafunzi na walezi kujumuika pamoja na kuwa na lengo moja la kufurahia Mungu anayowajalia katika maisha.

HOTUBA YA BABA ASKOFU.

Mtakatifu Yosefu anatuonesha fadhila kuu ya upendo na kutenda mema kwa yeyote yule. Alikubali kumpokea mtoto ambaye si wake na kumtunza mtoto na mama yake. Walezi wetu hapa Seminari wanawapokea wanafunzi kwa mapendo makubwa na kuwatunza bila kufahamu wazazi wao. Huku ni kufuata fadhila za Mtakatifu huyu. Wote tunahitajika kuwa watu wa Mungu, na kukubali majukumu yote tunayopewa mbele yetu, kama Mt. Yosefu. Tuombe Mungu tujaliwe na sisi kuyatunza mafumbo matakatifu, mafumbo ya ukombozi wetu, mwili na damu ya Kristo.

Seminary hii ni yetu sote, Askofu, walezi, walimu, wazazi na waamini wote. Hiki ndicho kituo kinachotulelea mapandre wetu wa baadaye. Tunaamini, hata mwanafunzi asipokuwa padre basi atakuwa mkristo mwema na raia mwema kwa nchi yetu.

MAFANIKIO
Mafanikio yapo kwa upande wa masomo, matokea ya kidato cha nne kwa mwaka huu yanaridhisha. Hii inaonesha ni kwa jinsi gani waalimu na wanafunzi wanavyoshirikiana.
Tumeanza ujenzi wa jengo la Maktaba ambalo juu yake kutakuwa na madarasa 4.
Pia tumeanza ujenzi wa dispensary ndogo ambayo tunategemea itakuwa msaada mkubwa sana kwa wanafunzi wetu na watu jirani.


 
Vijana wa Sakharani wakitumbuiza siku ya Mt. Yosefu Soni Seminary
Maandamano ya ibada mbele ya nyumba ya mapadre, Soni Seminary

MATATIZO
Matatizo yapo
1. uhaba wa fedha kwa ajili ya kuendesha shule, Misaada tunayotegemea imepungua kwa kiasi kikubwa.
2. ada inayolipwa haitoshelezi kabisa kufidia gharama za uendeshaji.Wazazi mnaimizwa kulipa ada kwa wakati.

- Wazazi katika siku hii ya Mt. Yosefu walichangia kiasi cha pesa taslimu na ahadi, Tshs Milioni 1.5 na tani 3.5 za cement. Huu ni mchango mkubwa katika kufanikisha maendeleo ya shule yetu. Bila kuwasahau Mama wa Shauri Jema pia walichangia kama kawaida yao, mchele, sukari, mafuta na vitu vingine vingi tu. WAWATA Chumbageni pia walichangia fedha.

SHUKRANI.
Tunawashukuru sana wazazi kwa kutoa michango yao na tunaomba waendelee na moyo huu, ili kwa pamoja tukiongozwa na mchungaji wetu Baba Askofu Anthony Bazi, Askofu wa Kanisa Katoliki Tanga, kuendelea kuiendeleza Seminary yetu, ambayo ndiyo alama ya kuendelea kwa kanisa letu Tanga, maana ndiyo sehemu ya uhakika wa kupata wachungaji siku za usoni.

Imetayarishwa na Pd. Richard Kimbwi