Mhashamu Askofu Maurus Komba ni askofu mzalendo wa kwanza kuliongoza
kanisa katoliki Tanga baada
ya Askofu Eugene C. Arthurs,
I.C.
Alizaliwa mwaka 1923 katika kijiji cha Mitambotambo
katika wilaya Mbinga mkoa wa Ruvuma. Alipata elimu ya msingi katika
shule msingi Litembo na baadaye alijiunga na shule za Peramiho na
Kigonsera kwa masomo ya sekondari. Baadaye alijiunga na Seminari
kuu ya Peramiho kwa masomo ya Falsafa na Teolojia. Alipewa daraja
la upadre tarehe 15 Julai, 1954.
Akiwa padre alifanyakazi katika parokia za Mbinga, Mkumbi na Mbangamao
katika jimbo la Mbinga na baadaye kama Paroko katika parokia ya
Peramiho na Songea katika jimbo la Songea.
Aliteuliwa na Baba Mtakatifu Paul VI kuwa Askofu
wa Jimbo la Tanga Machi
1969 na kuwekwa wakfu 15 Machi, 1970. Alifanyakazi kama Askofu wa
Tanga kwa muda wa miaka 18 mpaka alipostaafu kwa sababu za kiafya
mwaka 1987 na kurudi nyumbani kwao katika Jimbo la Mbinga. Alifariki
15 Machi 1996 na kuzikwa katika kanisa la parokia ya Mt. Alois Gonzaga,
Mbinga. |