KANISA KATOLIKI JIMBO LA TANGA TANZANIA

Kanisa Kuu

this page in english

Parish churches Tanga Diocese

KARIBU SANA

Tunakukaribisha kwenye tovuti yetu rasmi ya Jimbo Katoliki la Tanga lililo nchini Tanzania katika Afrika ya Mashariki.

Rudi Home page

Kanisa la zamani la Mt. Anton wa Padua
Masista/watawa wa shirika la COLU.
Kanisa la Parokia ya Amani.
Jengo la utangazaji la Radio Huruma.
Jengo la Ofisi za Jimbo.

MATUKIO NA PICHA

Matukia mengine

Radio Huruma,

Directory ya Jimbo

Sisi wana familia ya Jimbo la Tanga Tanzania tunapenda kuwakaribisha ndugu na marafiki zetu wote pote ulimwenguni kwenye tovuti hii rasmi ya jimbo letu ili tuweze kufahamiana na kuendelea kukuza mahusiano yetu kama watoto wa Mungu. Tumejitahidi tuwezavyo kukusanya habari nyingi ambazo zinawezesha ndugu wote ndani na nje ya jimbo kutufahamu. Uwezo wako wa kupitia kurasa za tovuti hii zitakuwezesha kufahamu historia ya jimbo letu hapo kale hadi sasa na pia kuzifahamu taasisi za jimbo letu, watumishi wake na miundo mingi ya jimbo ikiwa ni pamoja na kuifahamu jumuia yetu hai ya walei. Kwa vile jimbo letu linaendelea kukua kila iitwayo siku, basi yaliyomo ndani ya kurasa hizi hayatasita kubadilika kila baada ya muda. Kwa mantiki hii, usisite kutembelea tovuti yetu tena na tena kuweza kujifunza mengi yahusulo jimbo letu. Tovuti hii ni moja ya zana kadhaa za uinjilishaji ndani na nje ya Jimbo la Tanga. Zana hii imetumika kuweza kuwaunganisha wana Jimbo la Tanga na marafiki zetu pote ulimwenguni katika harakati kabambe za kuishi na kuitangaza Injili ya Kristu hadi pale Bwana Yesu atakaporudi mara ya pili katika utukufu wake.

Tunaendelea kuwaomba ndugu zetu wote muzidi kuendelea kutembelea tovuti yetu na muwe wawazi kutoa maoni na ushauri wenu kuhusu ubora wa tovuti yetu. Mawazo na ushauri wenu utaendelea kuiboresha zana hii. Kadhalika mtakapohitaji kuwasiliana moja kwa moja na Jimbo letu, taasisi zake, au watendaji wake, tovuti hii imejaribu kukuletea anuani pepe, anuani za posta, na pia namba za simu zitakazosaidia nia hiyo ya mawasiliano kufanyika wakati hitaji linapojitokeza. Uundwaji wa tovuti hii Jimbo Katoliki la Tanga umekuwa ni mrejesho wa kujiunga na jumuia kubwa ya ulimwengu kupitia katika teknolojia ya internet, teknolojia iliyotujia mwishoni mwa Karne ya Ishirini na kutuingiza ndani ya Karne ya Ishirini na Moja. Teknolojia hii imeufanya ulimwengu kuwa kijiji. Sisi wana jimbo la Tanga kama wanakijiji wa ulimwengu huu, tunaendelea kufaidika kwa kuwafahamu wanavijiji wa sehemu mbalimbali za ulimwengu na kadhalika nasi tunapaswa kujifahamisha kwa wanavijiji wengine kwa lengo la kushirikiana kuujenga Ufalme wa Mungu hapa duniani kama ilivyo kule mbinguni. Uundwaji wa tovuni hii na uwepo wake ni matokeo ya juhudi za askofu wetu wa jimbo na ukarimu wa wa mapadre, masista, mabruda, na walei walio ndani na nje ya jimbo. Tovuti hii imekuwa ni sokoni ambapo wanavijiji toka sehemu zote wanaweza kukutana na kusimuliana zimulizi na njozi za watoto wa Mungu.

Karibuni sana kufaidika toka kurasa hizi za tovuti hii. Hii ni tovuti yako.

KARIBUNI SANA!

-----------------

N.B: Ukiwa na swali lolote linalohusu ubora wa tovuti hii basi usitite kuwasiliana moja kwa moja na mkandarasi wa tovuti hii kupitia padre Richard Kimbwi katika Tuma Pepe.

edited_Agosti_2019

Officila sign-in.