PAROKIA YA MOYO MT. WA YESU
MKUZI TANGA
DEKANIA YA LUSHOTO
Parokia ya Moyo Mt. wa Yesu (2003) RATIBA YA IBADA: |
Moyo Mt. wa Yesu Nyumba ya mapadre |
|
HISTORIA YA PAROKIA
Parokia ya Mkuzi ipo ndani ya milima ya Usambara magharibi kilometa kadhaa toka mjini Lushoto kandokando ya barabara inayounganisha mji wa Lushoto na
vijiji vya Mlola, Kwekanga, na Malibwi. Mkuzi ipo katikati ya parokia za Gare na Kwai na kwa hivi karibuni imejongelewa na Parokia ya Mabughai. Hapo
awali Mkuzi ilikuwa ni kigango cha Parokia ya Kwai. Historia inakwenda nyuma zaidi kwamba Mkuzi ilikuwa ni kigango cha Parokia ya Gare kabla Kwai
haijakuwa parokia.
Tokea mwaka 1915 mapadre toka Parokia ya Gare walifika Mkuzi kwa huduma za kichungaji. Siku za baadaye wakati Kwai ilipotangazwa kuwa parokia
inayojitegemea, basi kigango cha Mkuzi kilikabidhiwa uongozi wa Parokia ya Kwai. Familia nyingi za ki-Katoliki zinazoishi maeneo ya Mkuzi zina mizizi
ya u-Katoliki wa muda mrefu kama vile ilivyo kwa Gare kwani familia nyingi za hapa zina mahusiano ya kiukoo na familia zilizo Gare.
Katika miaka ya karibuni, idadi ya waumini wa-Katoliki katika nchi ya Mkuzi imeongezeka sana kutoka pia na ongezeko la watu katika taifa. Katika mwaka
2003, Mkuzi ilitangazwa kuwa parokia inayotegemea yenyewe.
Wa-Katoliki watu wazima katika nchi ya Mkuzi wanazikumbuka kazi njema za uinjilishaji zilizofanywa na mapadre wamisionari wa ki-Rosmini kama vile Luigi
Cerana, I.C., Michael O’Shea I.C., Jim Polock, I.C. na Gerald Cunningham, I.C. Mapadre hawa katika muda mbalimbali walipendezwa kutolea nguvu zao
kuboresha maisha ya watu na imani Katoliki katika nchi ya Mkuzi. Kila mmoja wao alichangia kwa namna yake kuiboresha Mkuzi. Alipokuwa paroko wa Mkuzi,
padre Cunningham aliishi Kwai na kuja kufanya uchungaji Mkuzi kila siku. Anafahamika sana kwa kuweza kujenga nyumba ya mapadre na pia kujenga shule ya
ufundi seremala.
Ubora wa maisha ya imani Katoliki katika nchi ya Mkuzi na Gare unajionyesha katika idadi nzuri ya miito mitakatifu iliyojitokeza katika sehemu hiyo.
Shirika letu la masista wa Mama Yetu wa Usambara lina wanachama wengi masista tokea parokia hii.
Mapadre wazawa kutoka Parokia ya Mkuzi ni: Casmir Magwiza (1975) (R.I.P.), Richard Mshami (1981) (R.I.P.)
na John Sabuni (2001).