PAROKIA YA MT. YOHANE MBATIZAJI
DONGE TANGA
DEKANIA TANGA MJINI


A generic square placeholder image with a white border around it, making it resemble a photograph taken with an old instant camera


Parokia ya Mt. Yohani Mbatizaji (2022)
S.L.P 53, Tanga, Tanzania.
Donge

RATIBA YA IBADA:
JUMAPILI:
Misa 1: saa 12:30 Asubuhi.
Misa 2: saa 02:30 Asubuhi
Misa 3: saa 10:00 jioni (Misa ya watoto)

SIKU ZA JUMA;
Jumatatu hadi Jumamosi saa 12:15 Asubuhi

Mapadre:
Pd. Paulo Mshami: Paroko

parokia_chumbageni_mtanthoni_wa_padua

Mtakatifu Yohani Mbatizaji
somo wa Parokia.
Sherehe yake ni kila
Tarehe 24 Juni

parokia_chumbageni4

Ujenzi wa kanisa jipya
Donge

Nyumba ya Masista


Nyumba ya mapadre na eneo la kanisa

HISTORIA YA PAROKIA


Parokia ya Donge ipo kusini mashariki ya jiji la Tanga kilometa chache sana mashariki ya barabara inayounganisha jiji la Tanga na mji wa Pangani. Toka miaka ya mwishoni mwa 1980 na mwanzoni mwa1990 wakazi wa mji wa Tanga waliendelea kuongezeka kuleta changamoto la upanuzi za sehemu mpya ya makazi ya watu. Kutokana na hali hii, wakazi wengi wa Tanga walitaka kujipanua, walitafuta viwanja katika maeneo haya ya Donge ambayo yamo katikati ya vitongoji vya Usagara, Sahare kwa upande wa kaskazini na Mwambani upande wa kusini. Kwa asilia maeneo haya ya Donge yalikuwa ni maskani ya wenyeji wa miaka mingi wa maeneo haya ambao ni wa kabila la ki-Digo waliojishughulisha na ukulima mdogo mdogo wa mazao ya chakula na pia uvuvi mdogo katika pwani ya Bahari ya Hindi. Ujio wa wageni hawa waliotafuta sehemu za kujenga makazi ya kudumu, uliwafanya wenyeji wa maeneo haya kuuza mashamba yao kwa wageni hawa.
Ujio wa wageni hawa wakazi uliongezeka sana kuelekea miaka ya 1990 kati na hivi kuleta changamoto la mfumo wa kichungaji katika maeneo haya. Ni katika vuguvugu hili ndipo kulimfanya mheshimiwa padre Sean Madden, I.C aliyekuwa anaishi nyumba ya wa-Rosmini Mwambani kutafuta eneo la kujenga kigango katika eneo la Donge. Padre Madden alipata eneo la kununua toka kwenye shamba la mwenyeji mmoja wa hapo. Tokea hapo padre Madden alianza ujenzi wa jengo la kanisa katika kigango hiki ambacho toka siku za mwanzo kilikuwa chini ya Parokia ya Mtakatifu Teresia (Barabara Ishirini). Baada ya ujenzi wa kanisa na baadaye nyumba ya masista, padre Madden aliikikabidhi kigango hiki kwa parokia.
Katika mwaka 2005, kigango hiki cha Donge kilitoka kuwa kigango cha Parokia ya Mtakatifu Teresa kuja kuwa chini ya Parokia ya Mtakatifu Mulumba. Mwaka 2010 Baba Askofu Anthony Banzi alikiinua kigango hiki kuwa Parokia Tarajiwa. Bado mapadre wa Parokia ya Mtakatifu Mathias Mulumba waliendelea kutoa huduma za kichungaji hapo Donge.
Tokea mwanzo wa ujenzi wa kigango hiki cha Donge, juhudi zimekuwa zikifanyika kuweza kukifanya kigango hiki kuwa bora zaidi. Baada ya ujenzi wa jengo la kanisa, juhudi zilifanyika kuweza kukifanya kigango hiki kuwa na vuguvugu kubwa la kichungaji. Hatua za awali zilifanyika kujenga nyumba ambayo angekaa katekista. Baadaye wazo hili lilibadilika na kuifanya nyumba hii kuwa nyumba ya masista. Masista wa COLU walitumwa kufika hapa kuwa wakazi na utume wao umeendelea kuwa na chachu kubwa katika jumuia hii. Hatua nyingine katika uongozi wa Donge ulikuwa ni kujenga shule ya chekechea. Shule hii imekuwa ni kitalu bora cha malezi ya watoto wa maeneo ya Donge katika elimu ya awali.
Baadaye ujenzi wa nyumba ya mapadre ulianza na kukamilika, uchimbaji wa kisima cha maji umesaidia sana kupata maji ya kutosha katika ujenzi wa kanisa kubwa na la kisasa kwa ajili ya parokia kamili ya Donge. Kukamilika kwa Ujenzi wa miradi mikubwa na ule wa kanisa ambao unaendelea sasa kumetoa mwanya mkubwa wa kutangazwa rasmi Donge kuwa parokia mwaka 2022.