PAROKIA YA MT. MATHIAS MULUMBA
USAGARA TANGA
DEKANIA TANGA MJINI
![]()
RATIBA YA IBADA: |
![]() Mtakatifu Mathias Mulumba Mbele ya kanisa |
![]() |
Kanisa la zamani la parokia |
HISTORIA YA PAROKIA
Parokia ya Usagara ni moja ya parokia tatu katika jiji la Tanga. Parokia nyingine katika jiji hili ni Parokia ya Mtakatifu
Antoni wa Padua iliyo katika kitongo cha Chumbageni na parokia ya Mtakatifu Teresia iliyo kitongoji cha Barabara ya Ishirini.
Hadi mwaka 1987 waumini wengi wakaaji wa maeneo ya Usagara walikuwa wakipiga mwendo kwenda kupata huduma za ibada kwenye
parokia nyingine za mjini Tanga. Mwendo ulikuwa ni mkubwa kwa wengi waliokuwa na umri mkubwa na pia kwa watoto.
Katika miaka hiyo ya 1987 maeneo haya ya Usagara na Sahare yalipanuka mno kama makazi ya watu ambapo nyumba nyingi za kuishi
watu zilijengwa. Kukua huku wa makazi ya watu na ongezeko la waaumini wa-Katoliki, kulimsukukuma aliyekuwa paroko wa parokia
ya Mtakatifu Antoni mheshimiwa padre Gerard Smith, I.C. kutafuta eneo la kiwanja kwa ajili ya kujenga kanisa litakalowahudumia
wakazi wa maeneo haya. Eneo kubwa na zuri lilipatikana na mara moja padre Smith alianza ujenzi wa kanisa kubwa na zuri katika
eneo hili.
Mara baada ya ujenzi wa kanisa kukamilika, padre Smith aliendelea na ujenzi wa nyumba ya mapadre na tena nyumba ya masista
pamoja na jengo la shule ya awali kwa watoto. Baada ya ujenzi wote huo kukamilika, Mhashamu Askofu Telesphor Mkude
alilibariki jengo la kanisa hili Desemba 31, 1989 na kumteua Mtakatifu Matias Mulumba kuwa mlinzi wa kanisa hili.
Baba askofu Mkude alikiinua kigango cha Usagara kuwa parokia inayojitegemea Mei 25, 1990 na akamteua mheshimiwa
padre Casimir Shekibuah kuwa paroko wa kwanza wa parokia mpya.
Parokia ya Usagara imebarikiwa kuwa na utume wa masista wa shirika la Mama Yetu wa Usambara (COLU) ambao ni chachu kubwa
ya uinjilishaji kwa watu wa maeneo haya.
Ongezeko la watu katika maeneo ya vitongoji vya Usagara na Sahare mwishoni mwa Karne ya 20 kuendea mwanzo mwa Karne ya
21 umeendelea kuongeza idadi ya wa-Katoliki katika jiji la Tanga na katika vitongoji hivi vya Parokia ya Mtakatifu Matias
Mulumba. Ongezeko hili limeongeza changamoto katika utaratibu wa shughuli za kichungaji. Uongozi wa parokia hii chini ya
baba paroko wa sasa mheshimiwa padre Paul Mshami uliona kwamba kuna hitajiko la kuwa na jengo kubwa zaidi la kanisa
kukabiliana na ongezeko hili. Jengo la kanisa la sasa linauwezo wa kuchukua watu 200 tu na hivi kufanya ibada zote za
misa hapo parokiani kuwa na mbanano mkubwa. Hivi hitaji hili la kuwa na kanisa kubwa zaidi lilikubaliwa na uongozi wa
jimbo na siku ya Jumatano ya Majivu 2004 msingi wa jengo jipya la kanisa ndani ya eneo la parokia ulianza kuchimbwa.
Ujengaji wa jengo hili jipya la kanisa unazidi kuendelea na hadi kukamilika kwake litakuwa na uwezo wa kuwawezesha
waumini 1,200 kukaa ndani kwa wakati mmoja.
Waumini wa Parokia ya Usagara na uongozi wa parokia yao wamekuwa mstari wa mbele katika kuchangia gharama za ujenzi wa
jengo hili. Furaha ya waumini wa parokia hii ni kubwa mno kuweza kuwa na jengo hili zuri na la kisasa.
Padre mzawa wa Parokia ya Usagara ni: Paul Ngayomela, C.PP.S (2008).