MAFUNGO YA MAPADRE

JIMBO KATOLIKI TANGA 2008

Muwezeshaji wa Mafungo, Pd Maurus Shemdoe

Fr. Emmanuel Mavengero, mmoja wa washiriki

Mapadre wakijiaandaa kwa Misa

Pd. Joseph Shetui, Mmoja wa washiriki

 

Hili ni tendo linalofanyika kila mwaka katika Jimbo Katoliki la Tanga. Mafungo haya mara kwa mara ufanyika mwishoni mwa mwezi wa June na kuishia mwanzoni mwa mwezi Julai. Zaidi ya mapadre 50 uhudhuria mafungo haya. Mapadre hawa hugawanywa katika makundi mawili na kuwa na wiki mbili hakika za mafungo.

Mafungo haya yalifanyingi katika Seminary ndogo ya Soni.

Mafungo ya mapadre yanalengo la kuwapa mapdre nafasi baada ya kutafakari juu ya wito wao, na kusali na kuomba Baraka na neema za Mungu mwenyewe ili wawezi kuendelea kuliongoza kundi walilokabidhiwa na Bwana. Hii huwa ni nafasi ya pekee sana kwani kwa mwaka mzima mapdre hawakupata nafasi kama hii na kukutana na kupumzika na kusali.

Mafungo ya mwaka huu wa 2008 yalihudhuriwa pia na mapadre wote wa Jimbo la Zanzibar. Tunamshukuru pia Pd. Maurusi Shemdoe ambaye ndiye aliyekuwa muezeshaji katika mafungo haya. Ajabu amefanya kazi nzuri na tunamshukuru Mungu kwa hilo.

Kubwa lililojitokeza katika mafungo haya ni juu ya Utandawazi jinsi unavyohathiri imani za watu, na kazi kubwa waliyonayo mapadre wa kizazi hiki, kuendeleza imani katika dini kwa kizazi hiki ambacho daima kinaona imani ni kitu cha kufikirika tu, wao wanataka kitu halisi kinachoweza kuguswa, kuonwa na kukamatwa na mifumo yote ya fahamu.

Kazi yote ya kuhubiri neno la Mungu kweli inahitajika sala na neema ya pekee katika ulimwengu huu wa sasa.

Mwisho ni juu ya kuendeleza sala kwa mama Bikira Maria, Mama wa Mataifa ili Amani ipatikane katika Dunia yetu ya sasa, kwani hali bado siyo nzuri hasa katika baadhi ya mataifa duniani.

Na: Pd. Richard Kimbwi

Mapadre wakiwa kwenye picha ya pamoja, baada ya ibada

Pd. Joseph Mbena, mmoja wa washiriki