+ Pd. Bernard Chissi Wasifu wake


WASIFU WAKE

Fr. Bernard Chissi
Parents:
Father: Bernard Mageuza Chisi
Mother: Kerubina Severine Luambano

Date and Place of Birth:
Date of birth: October 1958 Peramiho, Village: Ruhuwiko - Namandizi, Ward: Ruhuwiko, District: Songea Mjini , Region: Ruvuma, Country: Tanzania

Deaconate and Priesthood
Deaconate: 1992
Priesthood: 24/June/1994

Education:
Primary School Std I-VII, Seconday education form I-VII
Philosophy, Two year course,, Theology, four years course,

Other Courses and Achievement:
Clinical Pastoral education 6 months course., Financial Accounting, one year course.
Working experience:
1994 - Diocesan Procurator
1999 - Parish Priest of Mlingano Parish

2011 Sabbatical year
Died May 2012

MAREHEMU PADRE BERNARD CHISSI
Tarehe 9 Mei 2012 mwenzetu mpendwa padre Bernard Chissi amefariki dunia katika hospitali ya Tumaini Tanga. Padre Chisi amezikwa siku ya Jumanne (Mei 15, 2012) kwenye makaburi ya mapadre wa jimbo la Tanga kule parokiani Kilole, Korogwe Tanga.
Baba Chissi ni mwenyeji wa parokia ya Mtindiro katika wilaya ya Muheza. Kwa miaka 12 mfululizo hadi kiangazi mwaka jana, padre Chissi alikuwa paroko wa parokia ya Mlingano. Baba Chissi alikuwa ni mchapa kazi hodari katika shamba la Bwana kule Mlingano na jimboni. Mchango wake katika uinjilishaji kule Mlingano na pia ujenzi wa parokia ni mkubwa mno.
Baada ya kuondoka parokia ya Mlingano mwaka jana, padre Chissi amekuwa katika kipindi cha sabatiko kwa muda mfupi katika tawa za Ligano na Hanga kule Songea kabla ya kurudi jimboni Tanga na kuendelea na sabatiko yake kule kituo cha kiroho Amani - Tanga.
Wiki mbili kabla ya kifo chake padre Chissi alipata "stroke" akiwa kule Amani na kuletwa katika hospital ya Tumaini Tanga kwa tiba mpaka alipofariki dunia.

Tuiombee roho ya marehemu padre Bernard Chisi na roho za marehemu wote waamini mapumziko ya milele mbinguni. AMINA

catholic diocese of Tanga

© 2024