WASIFU WAKE
Pd. Casmir Shekibuah alizaliwa Tarehe: 28/01/1955,
Alipewa daraja takatifu la upadre tarehe: 10/12/1980,
Alifariki tarehe: 23/11/2004 na kuzikwa katika makaburi ya mapadre Jimboni Tanga, huko parokiani Kilole.
Katika utume wake anakumbwa zaidi kwa mchango wake katika muziki wa kanisa. Ametunga nyimbo nyingi ambazo hadi sasa
zinatumika katika ibada katika kanisa katoliki. Kipaji chake katika muziki wenye maadhi ya kabila la kisambaa ulifanya muziki huo kupendwa sana na wengi.
Alifariki mwaka mmoja kabla ya kutimiza miaka 25 ya utume wake katika kanisa kama padre.
Kabla ya kufariki kwake akiwa parokiani Muheza alikokuwa akijiuguza alikwishaanza kuandaa maandalizi ya kusherekea Jubilei yake
ya miaka 25 ya utume katika kanisa kwa kutunga nyimbo mbalimbali ambazo zingeimbwa katika ibada hiyo.
Padre Richard Kimbwi anasimulia kuwa aliombwa na Pd. Shekibuah kuwa ajiandaye kuifundisha kwaya ya parokiani Muheza kwa ajili ya maandalizi
hayo ya Jubilei. Kabla ya kupokea nyimbo hizo za maandalizi, hali ya Padre Shekibuah haikuwa nzuri na ilitia shaka sana juu ya
maandalizi hayo. Pd. Kimbwi anasimulia kuwa wakiwa wanasubiri Pd. Shekibuah apate nafuu ili zoezi la maandalizi lianze mara Mungu
naye alitimiza mapenzi yake na kumuita kwake.
Raha ya milele umpe Ee Bwana: na Mwanga wa milele umuangazie
Apumzike kwa Amani : Amina.
catholic diocese of Tanga © 2024
|