WASIFU WAKE
+ Padre Ignas Safari alizaliwa mwaka 1938,
Alipata daraja takatifu la upadre tarehe 26/06/1972,
Alifariki tarehe 20/12/1991 akiwa ni padre wa kwanza mwanajimbo kufariki na pia padre wa kwanza kufungua na kuzikwa katika
shamba la kuzikia mapadre parokiani Kilole wilayani Korogwe Tanga.
Alidumu katika utume wake kama padre kwa muda wa miaka 19.
Mbele za Bwana hakuna mtenda kazi wa muda mrefu na mfupi, kwani waliotoka asubuhi, alasiri na jioni kwenda kufanyakazi katika shamba
lake bado Bwana wa shamba aliwasawazisha katika kuwapatia ujira wote.
Tunamshukuru Mungu kwa utume wa Pd. Safari katika jimbo letu la Tanga.
Raha ya milele umpe ee Bwana: Na mwanga wa milele umuangazie.
apumzike kwa amani: Amina.
catholic diocese of Tanga © 2024
|