+ Pd. John Chambi Wasifu wake


WASIFU WAKE

Marehemu Padre John Chambi alizaliwa Desemba,1957 na wazazi baba David Chambi na mama Elizabeth Kilua katika kijiji cha Gare wilayani Lushoto mkoani Tanga, Tanzania.

ELIMU
Mwaka 1965 - 1971 alisoma shule ya msingi Gare kuanzia darasa la I - VII.
1972 - 1975: kidato cha I - IV katika Seminari ndogo ya Mt. Peter huko Morogoro, Tanzania.
1976-1978: alisoma masomo ya Falsafa (Philosophy) huko seminari kuu ya Kibosho Moshi, Tanzania.
1981: alifanya mwaka wa uchungaji katika parokia ya Mt. Anthony wa Padua Chumbageni Tanga, Tanzania.
1978-1982: alisoma masomo ya Teolojia (Theology) katika seminari kuu ya Kipalapala huko Tabora, Tanzania.

USHEMASI NA UPADRE
June 29, 1982: alipata daraja la ushemasi katika kanisa la Mt. Anthony wa Padua Chumbageni Tanga, Tanzania.
November 25, 1982: alipata daraja takatifu la upadre huko parokiani Gare Lushoto Tanga, Tanzania

ELIMU ZAIDI
1988 -1990: Master’s Studies in Scripture at Catholic University of East Africa (CUEA) in Nairobi, Kenya

UTUME
1982-1985: msaidizi wa paroko parokiani Lushoto, Tanga, Tanzania
1985 – 1987: alifanya utume Seminari kuu ya Kibosho kama mwalimu na mlezi huko Moshi, Tanzania
1991 – 1992: alifanya utume Seminari kuu Segerea kama mwalimu na mlezi huko Dar Es Salaam, Tanzania
1992 – 1997: alikuwa Chaplain COLU Sisters katika Convent ya Rangwi huko Lushoto, Tanzania
1997 – 2002: alihudumu kama Formator katika nyumba ya malezi ya vijana wanaotaka kujiunga na upadre, huko Shashui, Soni, Lushoto.
2002 – 2006: alikuwa paroko katika parokia ya Kongoi Lushoto, Tanga, Tanzania.
2006 - October 16, 2016: mpaka anafariki alikuwa Chaplain COLU Sisters huko Convent ya Kwamndolwa Korogwe, Tanga, Tanzania.

Alifariki ghafla Oktoba 16, 2016 akiwa Kwamndolwa kwenye kituo chake cha kazi, na kuzikwa katika makaburi ya mapadre parokiani Kilole Korogwe Tanga. Ameweza kulitumikia kanisa kama padre kwa muda wa miaka 34.

Raha ya milele umpe ee Bwana: Na mwanga wa milele umuangazie.
Apumzike kwa amani: Amina.

catholic diocese of Tanga

© 2024