WASIFU WAKE
Kuzaliwa:
Mheshimiwa Padre Maurus Bernard Shemdoe alizaliwa 10/07/ 1970 katika kijiji MALINDI, LUSHOTO
Wazazi wake:
Baba Bernard Festus Shemdoe na Mama Celina Mansuetus
Ubatizo:
09/08/1970 parokiani Rangwi, namba yake ya ubatizo ni 1667 ktk Kitabu cha pili.
1980 - 1986 Alipata elimu yake ya Msingi katika shule ya msingi Malindi – Lushoto
MAFUNZO YA UPADRE
1987 - 1992 Padre Maurus Alijiunga na seminari ndogo ya Mt. Josef, Soni masomo ya sekondari na malezi ya upadre
1993 - 1995 Baada ya kufaulu vizuri masomo kidato cha 4 Alijiunga na seminari ndogo ya Mt. Petro Morogoro kwa masomo ya kidato cha Tano na Sita.
1995 - 1996 Alifanya mwaka wa malezi ya kiroho pale Gare kwa kujiandaa na mafunzo ya seminari kuu.
1996 - 1998 Alijiunga na seminari kuu ya KIBOSHO huko Moshi kwa masomo ya Falsafa.
1998 – 2003 Alipata mafunzo ya Teolojia katika seminari kuu ya Mt. Karoli Lwanga Segerea huko Dar es Salaam
2001 - 2002 Alifanya mwaka wa kichungaji katika Seminari ndogo ya Mt. Josef Soni Lushoto.
25/01/2003 Alipata daraja la ushemasi katika seminari kuu ya Mt. Karoli Lwanga Segerea Dar es Salaam
22/08/2003 Alipata Daraja Takatifu la Upadre katika Parokia yake ya Malindi Lushoto Kanisa.
2005 - 2007 Miaka miwili baada ya upadrisho wake, alitumwa na jimbo kwenda kuchukua masomo ya uzamili (Masters) katika Chuo Kikuu cha Maaskofu
wa Afrika ya Mashariki -CUEA – Nairobi Kenya
UTUME WAKE
2003 - 2004 Paroko msaidizi katika parokia hii ya Kilole
2004 - 2005 Mlezi wa Kiroho katika seminari ya Mt. Petro jimbo la Morogoro
2007 - 2010 Mlezi wa Kiroho katika seminari ya Mt. Josef jimboni Tanga
2010 - 2015 Paroko msaidizi parokia ya Mt. Mathias Mulumba Tanga na wakati huohuo Mlezi wa kiroho wa Wagonjwa na Wafungwa.
2015 – 2019 Mlezi wa kiroho katika Chuo cha Askofu Mkuu James (AJUCO) chuo kishiriki cha SAUT huko SONGEA
2019 - mpaka siku ameitwa na Bwana: alikuwa ni mlezi wa kiroho katika vyuo viwili:Songea Catholic Institute of Technical Education Na Peramiho
Institute of Health and allied Sciences vyote vipo Songea.
Aidha Padre Maurus Shemdoe Katika utume wake amekuwa na kipaji cha utume wa kutoa mafungo kwa makundi mbalimbali ya Waumini na hasa Watawa.
Raha ya milele umpe ee bwana ………Apumzike kwa Amani……
UGONJWA NA UMAUTI
Kipengele hiki naomba kumkaribisha Padre mkuu wa Chuo kiitwacho Songea Catholic Institute of Technical Education na ambaye alikuwa anaishi naye
atoe maelezo mafupi kisha nitaendelea na shukrani.
Raha ya milele umpe ee bwana …Apumzike kwa Amani……
SHUKRANI:
Jimbo Katoliki la Tanga linamshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha ya Padri Maurus Shemdoe, na kwa utume wake mkubwa aliufanya katika Jimbo letu la
Tanga na kanisa la Tanzania kwa ujumla kwani huko Jimbo la Songea alitumwa Baraza la Maaskofu Tanzania.
Tunamuomba Mungu amzawadie furaha ya milele kwa utume wake huo uliotukuka
Kwa namna ya pekee tunamshukuru Baba Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea kwa kumpokea na kumfanya padre wetu na kumshirikisha utume katika Jimbo lake
na upendo aliupata kwa waumini wa Jimbo la Songea. Pia Tunawashukuru Mapadre, Watawa na Walei wa Jimbo la Songea kwa upendo wenu wa kumsindikiza
padre wetu mpka hapa kwenye nyumba yake ya milele. Mungu awabariki sana.
Tunawashukuru uongozi mapadre waliokuwa wanaishi naye Padre Longino na wenzake kwa kujitahidi kuokoa maisha yake alipopatwa na shida ile na kwa
upendo wote mliompatia wakati wa utumishi wake.
Tunawashukuru madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Songea na hospital ya Peramiho, na kumsaidia katika ugonjwa wake na hasa Dr. Mama ………………………..
kwa majitoleo yako katika harakati za kuokoa maisha yake na kumtayarisha vizuri katika maziko yake.
Nanyi wageni wetu mliotufikia kutoka mbali na karibu mkiongozwa na Baba Askofu Titus Mdoe wa Jimbo la Mtwara, mmetufariji sana kwa ujio wenu.
Umati huu toka sehemu mbalimbali zinatuonyesha upendo mkubwa aliougawa padre wetu kwa watu wa Mungu. Mungu awabariki sana kwa upendo wenu kwa
padre wetu.
WALIOTUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA ASKOFU MTEULE.
Jimbo Katoliki la Tanga limepokea salamu za rambirambi kupitia kwa Askofu mteule toka watu mbalimbali wenye mapenzi mema wakiwemo,
Mapadre: Severine Yagaza, Augustine Temu, Paul Shirima, Richard Kajiru, Severine Msigiti, Richard Kimbwi, Peter Kagaba, James Kabosa wakiwa
nje ya nchi.
catholic diocese of Tanga © 2024
|