+ Pd. Patrick Daniel Mngano Wasifu wake


WASIFU WAKE

Mrehemu Padre Daniel Patrick Mngano alizaliwa Juni 1968 na wazazi baba Daniel Mngano na mama Tansila Soai katika kijiji cha Kwemivulu Kongoi, Lushoto Tanga Tanzania.

ELIMU
1982 – 1988: Alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Mgwashi Kongoi Lushoto.
1989 – 1992: Alisoma elimu ya Sekondari kuanzia kidato cha I – IV katika shule ya sekondari Galanos iliyoko Tanga mjini.
1993 – 1995: Aliendelea na elimu ya sekondari kwa kidato cha V – VI huko Pugu Secondary School.

MAFUNZO YA UPADRE
1995 - 1996: Alijiunga na nyumba ya malezi huko Gare, Lushoto, Tanzania
1996 – 1998: Alijiunga na seminari kuu Ntungamo huko Bukoba, Tanzania, kwa masomo ya Falsafa
2001 – 2002: Alifanya mwaka wa kichungaji katika seminari ndogo ya jimbo Soni Seminary School huko Soni, Lushoto, Tanga, Tanzania.
1998 – 2003: Alisoma masomo ya Theolijia (Theology) katika seminari kuu Kipalapala, Tabora, Tanzania

DARAJA LA USHEMASI NA UPADRE
January 25, 2003: alipata daraja la Ushemasi katika Seminari kuu Kipalapala Tabora, Tanzania
August 29, 2003: alipewa daraja takatifu la upadre huko parokiani Kongoi, Lushoto.

MASOMO ZAIDI
2004 – 2007: alitunikiwa cheti cha Diploma katika uwanja wa Elimu huko Mwenge University College of Education, Moshi, Tanzania

UTUME WAKE
2003 - 2004: Paroko msaidizi parokiani Manundu Korogwe, Tanga, Tanzania
2007: Mwalimu na mlezi katika seminari ndogo ya jimbo Soni
Agosti 2013: Gombera wa Soni Seminari
October 2013: Paroko msaidizi parokiani Kilole, Korogwe. Na muda mfupi alitumwa kuwa Paroko wa parokia ya Mazinde Ngua Mombo.
Alianza kuugua akiwa katika parokia hii ya Mazinde Ngua. Kwa mda mrefu aliangaikia zaidi afya yake.

KIFO
Tarehe 12 Novemba 2018 Mungu alimwita katika makao yake ya milele akiwa amefanya utume kama padre kwa muda wa miaka 15.
Mwili wake unalala katika makaburi ya mapadre parokiani Kilole Korogwe Tanga.

Raha ya milele umpe ee Bwana: Na mwanga wa milele umuangazie.
Apumzike kwa amani: Amina.

catholic diocese of Tanga

© 2024