+ Pd. Peter Amandrus Mapunda Wasifu wake


WASIFU WAKE

Marehemu Padre Peter Amandrus Mapunda alizaliwa Oktoba 1970 na wazazi baba Amandrus J. Lwanda na mama Adelhelma Cassian katika kijiji cha Mpakani, Kerenge wilayani Muheza, Tanga, Tanzania.

ELIMU
1978 - 1979: alipata elimu ya awali (Kindergarten) huko Bwembera Kihuhi, Muheza Tanga Tanzania
1979 – 1985: alipata elimu ya msingi kuanzia darasa la I-VII katika shule msingi Bwembera Kihuhi, Muheza Tanga, Tanzania

ELIMU YA UPADRE
1987 - 1991: Alijiunga na seminari ndogo ya jimbo Soni Seminari kuanzia Pre-Form I - IV.
1992 – 1994: Kisha alijinga na Seminari ya Mt. Peter huko Morogoro kwa elimu ya kidato cha V – VI.
1994 - 1995: Alijiunga na nyumba ya malezi Gare Lushoto Tanga.
1996 - 1998: Alijiunga na masomo ya Falsafa katika Seminari kuu ya Ntungamo huko Bukoba, Tanzania
2000 - 2002: Alifanya mwaka wa kichungaji huko Soni Seminary Soni Lushoto, Tanzania
1998 - 2002: Alijiunga na masomo ya Theolojia katika seminari kuu ya Segerea huko Segerea, Dar Es Salaam, Tanzania

USHEMASI NA UPADRE
August 17, 2002: alipewa daraja la ushemasi huko parokiani Potwe, Tanga, Tanzania
January 17, 2003: alipewa daraja la upadre huko parokiani Potwe, Tanga, Tanzania

ELIMU ZAIDI
2003: Alipata mafunzo ya Charismatic Renewal huko Kampala, Uganda

UTUME WAKE
2003 – 2004: paroko msaidizi katika parokia ya Mt. Anthony wa Padua Chumbageni Tanga, Tanzania
2004 – 2006: alihudumu katika nafasi ya Diocesan Procurator jimboni Tanga.
2006 – 2009: alihudumu kama paroko msaidizi katika parokia ya Malindi Lushoto Tanga Tanzania
2010 - 2015: alikuwa paroko msaidizi katika parokia ya Kongoi Lushoto Tanga Tanzania
2015 - 2016: paroko msaidizi parokia ya Kwediboma, Tanga, Tanzania
2016 - kifo: Paroko parokia ya Kwediboma, Tanga, Tanzania

KIFO
Marehemu Padre Peter Mapunda alifariki Februari 11, 2020 baada ya kuugua ghafla japokuwa kwa muda mrefu alisumbuliwa na moyo. Aliweza kutumikia utume wake kama padre kwa muda wa miaka 17.
Mwili wake unapumzika katika makaburi ya mapadre parokiani Kilole Korogwe Tanga Tanzania.

Raha ya milele umpe ee Bwana: Na mwanga wa milele umuangazie.
Apumzike kwa amani: Amina.

catholic diocese of Tanga

© 2024