WASIFU WAKE
Marehemu Padre Peter Rodoussakis alizaliwa Mei 1958 na wazazi baba Alex Alecos Rodoussakis na mama Angelina Hendrish Laurich
katika kijiji cha Gare huko wilayani Lushoto, Tanga, Tanzania
ELIMU
1964 – 1965: alipata elimu ya awali (Kindergarten) huko shule ya msingi Gare Lushoto.
1966 – 1971: alisoma elimu ya msingi darasa la I-VII katika shule msingi Gare Lushoto.
MAFUNZO YA UPADRE
1972 - 1975: alijiunga na seminari ndogo kidato cha I - IV katika seminari ya Mt. Peter Morogoro, Tanzania
1976 - 1978: alijiunga na masomo ya Falsafa (Philosophy) seminari kuu Kibosho Moshi, Tanzania
1981: Alifanya mwaka wa kichungaji katika parokia ya Mt. Theresa bar.20 Tanga, Tanzania
1978 - 1982: alisoma masomo ya Theolojia (Theology) katika seminari kuu Kipalapala Tabora, Tanzania
MASOMO ZAIDI
1979: Aliitimu katika ufundi wa Mechanical Engineering for Diesel Engines
1979: Aliitimu katika fani ya Industrial Painting
USHEMASI NA UPADRE
Juni 29, 1982: alipewa daraja la ushemasi katika parokia ya Mt. Anthony wa Padua Chumbageni Tanga, Tanzania
Novemba 25, 1982: alipata daraja takatifu la Upadre huko parokiani Gare, Lushoto Tanga, Tanzania
UTUME WAKE
1982 – 1983: Alihudumu kama paroko msaidizi katika parokia ya Muheza, Tanga, Tanzania
1983 – 1985: alikuwa paroko msaidizi parokia ya Mlingano Muheza Tanga, Tanzania
1985: Paroko msaidizi parokia ya Malindi Lushoto.
1986 – 1989: paroko msaidizi parokia ya Hale.
1989 – 1992: paroko msaidizi parokia ya Kongoi Lushoto.
1992 – 1997: Paroko parokia ya Pangani
1997 – 1999: Paroko parokia ya Mlingano.
1999 – 2005: paroko msaidizi parokia ya Malindi Lushoto.
2005 – 2009: Paroko msaidizi parokia ya Maramba.
2009: Paroko msaidizi parokia ya Mt. Anthony wa padua Chumbageni Tanga, Tanzania
2010: alianza kuugua akiwa paroko msaidizi katika parokia hii ya Chumbageni.
2011: alihamia kwenye makao ya Askofu akiwa anaendelea na matibabu yake huko Raskazoni Bishop’s House Tanga, Tanzania.
KIFO
Akiwa Dar Es Salaam kwa matibabu yake aliruhusiwa kurudi nyumbani Tanga. Wakati jimbo linajiandaa kumtuma dereva kwenda
kumchukua kurudi nyumba kwa ruhusa hiyo ya hospitali mara hali yake ilibadilika ghafla. Baada ya muda mfupi tu ujumbe ulitumwa
jimboni kuwa padre Rodoussakis alishafariki hii ilikuwa ni Mei 25, 2015.
Padre Peter Rodoussakis amefariki akiwa amefanyakazi ya utume katika kanisa kwa muda wa miaka 33.
Tunamshukuru Mungu kwa utume wa padre Peter
katika kanisa jimboni Tanga.
Raha ya milele umpe ee Bwana: Na mwanga wa milele umuangazie
Apumzike kwa amani: Amina.
catholic diocese of Tanga © 2024
|