+ Pd. Richard Joseph Mshami Wasifu wake


WASIFU WAKE

Marehemu Padre Richard Mshami alizaliwa July 1953 na wazazi baba Joseph Mshami na mama Maria Tupa katika kijiji cha Mkuzi wilayani Lushoto Tanga Tanzania.

ELIMU
1963 – 1970: alipata elimu ya msingi darasa la I – VII katika shule msingi Kionwa Mkuzi, Lushoto, Tanga, Tanzania.
Baada ya kumaliza elimu ya msingi alijiunga na Seminari ndogo ya Mt. Peter huko Morogoro kwa masomo ya sekondari kuanzia mwaka 1971 – 1974 kwa kidato cha 1 – IV.
1975 – 1976: alijiunga na Seminari kuu ya Kibosho Moshi kwa masomo ya Falsafa (Philosophy)
1980: alifanya mwaka wa kichungaji parokiani Gare Lushoto Tanga.
1977 – 1981: alisoma masomo ya Thelojia (Theology) katika seminari kuu ya Kipalapala Tabora Tanzania

USHEMASI NA UPADRE
June 9, 1981: alipewa daraja la ushemasi katika kanisa la Mt. Anthony wa Padua (Cathedral) Tanga, Tanzania
November 22, 1981: alipata daraja takatifu la upadre katika kanisa la Mt. Anthony wa Padua (Cathedral) Tanga, Tanzania

UTUME WAKE KATIKA KANISA
1981 – 1984: alihudumu kama paroko msaidizi katika parokia ya Mlingano, Tanga, Tanzania
1984 – 1987: paroko msaidizi parokiani Kilole Korogwe.
1987 – 1988: paroko msaidizi katika parokia ya Lushoto.
1988 – 1992: paroko msaidizi parokia ya Mt. Theresia wa mtoto Yesu Bar.20 Tanga, Tanzania
1992 – 1997: paroko parokia ya Magoma, Korogwe, Tanzania.
1997 – 2002: Diocesan Director for Apostleship of the Sea in Tanga, Tanzania
2002 - 2009: paroko parokia ya Malindi, Lushoto, Tanga, Tanzania
2009 - 2011: paroko msaidizi parokia ya Mkuzi, Lushoto, Tanga, Tanzania
2011 - 2014: paroko msaidizi parokia ya Mlingano, Tanga, Tanzania
2014 - March 10, 2021: Paroko parokia ya Mlingano, Tanga, Tanzania

KIFO
Marehemu Padre Richard Mshami aliugua kifua kwa muda mrefu. Siku za mwisho wa uhai wake ililazimika kulazwa hosipitalini huko Dar Es Salaam. Machi 10, 2021 Mungu alimuita mpendwa wetu Padre Richard Mshami katika makao yake ya milele mbinguni.
Marehemu Padre Richard Mshami alizikwa siku ya Jumatano Machi 17, 2021 kwenye makaburi ya mapadre jimbo parokia ya Kilole, Korogwe.
Tunamshukuru Mungu kwa utume wa Padre Richard Mshami jimboni Tanga. Ameweza kulitumikia kanisa kama padre kwa muda wa miaka 40.

Raha ya milele umpe ee Bwana: Na mwanga wa milele umwangazie.
Apumzike kwa amani: Amina.

catholic diocese of Tanga

© 2024