+ Pd. Vincent Matoyoo Ushaki Wasifu wake


WASIFU WAKE

Marehemu Padre Vincent Ushaki alizaliwa Novemba 1931 na wazazi baba Joseph Matoyoo Ushaki na mama Augustina Morio Namfua katika kijiji cha Kitirima Mkuu ROMBO KILIMANJARO TANZANIA.

ELIMU
1945 – 1952 alipata elimu ya msingi katika shule msingi Mkuu Rombo.
1953 – 1956 alijiunga na elimu ya sekondari huko Singachini, St. Patrick College.
1953 – 1956 alisoma masomo ya ualimu huko Moshi Teachers Training College Singachini
1959 – 1960 alijiunga na Ukiriguru Agricultural Training Institute – Morogoro
1962 – 1963 alipata elimu ya falsafa huko St. Thomas Aquinas – Morogoro.
1964 – June 1968 alisoma masomo ya Theolijia katika seminari kuu Kipalapala

USHEMASI NA UPADRE
29.06.1968: Alipata daraja la ushemasi katika parokia ya Mt. Anthony wa Padua (Cathedral) Chumbageni Tanga.
08.12.1968: alipata daraja takatifu la upadre katika parokia ya Mt. Anthony wa Padua (Cathedral) Chumbageni Tanga.

UTUMISHI WAKE
1969 paroko msaidizi katika parokia ya Kilole Korogwe.
1969 – 1970 paroko msaidizi parokia ya Kwediboma.
1970 – 1971 paroko msaidizi na mwalimu wa shule ya makatekista Kwai Lushto Tanga.
1971 Paroko msaidizi parokiani Kilole Korogwe Tanga.
1971 – 1973 Paroko msaidizi parokiani Gare Lushoto
1973 – 1980 Paroko parokia ya Mt. Theresia wa mtoto Yesu Bar.20 Tanga.
1980 – 1982 Paroko parokia ya Lushoto
July 1982 – December 1982: Uaskofuni Tanga.
January 1983 – June 1992: Paroko parokia ya Muheza Tanga.
July 1992 – December 1996 Paroko msaidizi Mt. Anthony wa Padua Chumbageni Tanga.
December 2010 Paroko msaidizi parokia ya Mlingano.

KIFO
Marehemu Padre Vincent Matoyoo Ushaki alifariki ghafla November 13, 2017. Siku za karibuni kabla ya kifo chake alikuwa anasumbuliwa na malaria. Siku hiyo ya kifo chake aliamka na kwenda kituo cha afya kilichopo karibu na parokia ya Mlingano kwa lengo la kupima malaria. Baada ya majibu kuwa vipimo havikuonesha chochote aliondoka hapo akilalamika kuwa ni lazima aende Tanga mjini kwa vipimo zaidi. Akiwa tayari amewasha gari lake kuelekea Tanga mjini alishindwa kuliondoa gari hilo, ndipo watu waliopo kituoni hapo walimsaidia kumtoa kwenye gari na kumrudisha tena kituoni. Baada ya muda mfupi madaktari wakijaribu kuokoa maisha yake, ndivyo Padre Ushaki alivyotuacha.

Marehemu Ushaki mwaka huo aliofariki alikuwa anajiandaa pia kwa jubilei yake ya miaka 50 ya upadre ambayo angeisherehekea mwaka uliofuata. Lakini hata hivyo mara nyingi alisikika akionesha kutokuwa na hakika ya kufikia jubilei hiyo kwa sababu ya kuuguaugua mara kwa mara. Mungu amemwita kwake akiwa na miaka 49 ya utume katika kanisa.

Raha ya milele umpe ee Bwana: Na mwanga wa milele umuangazie.
Apumzike kwa amani: Amina.

catholic diocese of Tanga

© 2024