WASIFU WAKE
+ Marehemu Padre Vitus Nkondora alizaliwa Septemba 1941 na wazazi baba Gregory K. Nkondora na mama Lucia John katika kijiji cha Mandera, Bagamoyo
Tanzania.
ELIMU
1950 - 1955: alipata elimu ya msingi darasa la I - IV katika shule msingi Mandera Bagamoyo, kisha Old Korogwe Tanga, pia na Kwediboma Handeni
na mwisho huko Turiani Morogoro.
1956 – 1961: alijiunga na darasa la V - X huko seminari ya Mt. Peter Bagamoyo, Tanzania.
1962 – 1963: alisoma darasa la XI - XII katika seminari ndogo ya Nyegezi Mwanza, Tanzania
1964 – 1970: alisoma masomo ya Falsafa (Philosophy) na Theolojia (Theology) katika seminari kuu ya Kipalapala Tabora, Tanzania
USHEMASI NA UPADRE
December 1969: alipata daraja la ushemasi katika kanisa la Mt. Anthony wa Padua (Cathedral) Chumbageni Tanga, Tanzania
December 6, 1970: alipata daraja takatifu la upadre katika parokia ya Lushoto Tanga, Tanzania
MASOMO ZAIDI
1980 – 1981: Master in Spiritual Theology at Maryknoll School of Theoloy in Maryknoll, NY (USA)
UTUME WAKE
1970 - 1972: Paroko msaidizi parokiani Potwe.
1972 - 1975: Paroko msaidizi parokiani Kwai Lushoto.
1975 - 1976: Paroko parokia ya Kwai Lushoto.
1977 - 1980: Paroko parokia ya Lushoto.
1981 - 1989: Mwalimu na mlezi katika Spiritual seminari kuu ya Segerea Dar Es Salaam, Tanzania.
1989 - 1995: paroko parokia ya Mt. Anthony wa Padua (Cathedral) Chumbageni Tanga, Tanzania.
1989 - 1995: Diocesan Vicar General in Tanga, Tanzania.
1995 - 2000: Spritual Director seminari ndogo ya Jimbo Soni Seminary, Tanzania.
2000 - 2002: Lecturer and Spiritual Director seminari kuu Segerea Dar Es Salaam, Tanzania.
2002 - : Paroko parokia ya Mkuzi, Lushoto, Tanzania.
2015 : paroko msaidizi parokiani Potwe.
2017 : Uaskofuni Raskazoni Tanga, Tanzania.
KIFO
Marehemu Padre Vitus Nkondora alifariki January 31, 2019 katika hospital ya jimbo Tumaini Tanga baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Aliweza pia kulitumikia jimbo kwa muda wa miaka 49 ya upadre wake.
Raha ya milele umpe ee Bwana: na mwanga wa milele umuangazie.
Apumzike kwa Amani: Amina.
catholic diocese of Tanga © 2024
|