+ Msgr Ernest Andrea Seng'enge Wasifu wake


WASIFU WAKE

Mons. Ernest Andrea Seng'enge alizaliwa tarehe, 26/11/1949 katika Kijiji cha Kwadoe, Kata ya Sakharani, Wilaya ya Lushoto, Mkoa wa Tanga. Mons. Ernest Andrea Seng'enge ni mtoto wa tatu kati ya watoto saba wa Mzee Andrea Seng'enge na Mama Anna Bakari.

MAISHA YA SAKRAMENTI:-
Alipata Sakramenti ya Ubatizo tarehe 02/02/1969, LB: IX-462, Gare, alibatizwa na Pd.J. Matur. Msimamizi ni Adolf, Sakramenti ya Komunyo tarehe 26/4/1970 na Sakramenti ya Kipaimara tarehe 08/11/1970, katika Parokia ya Gare.

ELIMU:-
Elimu ya Msingi ng Sekondari:-
Mons, Ernest Andrea Seng'enge alisoma Shule zifuatazo:-
1963-1966:- Darasa la 1-IV, katika Shule ya Msingi Kwalei-Sakharani
1967-1969:- Darasa In V-VII, katika Shule ya Msingi ya Kwemvumo-Sakharani
1970:- Darasa la VII, Shule ya Msingi Fumbai/ Kisiwani-Soni
1971-1974:- Kidato cha I-IV, katika Seminary ya Mt.Peter-Morogoro.

MALEZI NA MAJIUNDO YA UPADRE:-
Mons. Ernest Andrea Seng'enge, Baadaye alijisikia kuitwa kumtumikia Mungu katika Daraja Takatifu ya Upadre. Hivyo alisoma na kupata malezi ya majiundo katika Seminari Kuu zifuatazo:- Seminari ya Kibosho/Moshi:-
Mwaka 1975-1976, Mons. Ernest Andrea Seng'enge alijiunga na Seminari Kuu ya Kibosho/ Moshi na kuhitimu masomo ya Falsafa.
Seminari Kuu va Kipalapala Tabora:-
Mwaka 1977-1981, Mons. Ernest Andrea Seng'enge alijiunga na Scminari Kuu ya Kipalapala kwa masomo ya Tauhidi/Teolojia.
Mwaka 1980 alifanya mwaka wa Kichungaji katika Parokia ya Kanisa Kuu la Mt. Antoni wa Padua, Chumbageai Tanga.

DARAJA TAKATIFU LA USHEMASI:-
Tarehe 09 Juni,1981, Mons. Ernest Andrea Seng'enge alipewa Daraja Takatifu la Ushemasi, katika Kanisa Kuu la Mt. Antoni wa Padua, Chumbageni Tanga na Mhashamu Askofu Maurus Komba aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Ia Tanga.

DARAJA TAKATIFU LA UPADRE:- Tarehe 25 Novemba,1981, Mons. Ernest Andrea Seng'enge alipewa Daraja Takatifu la Upadre katika Parokia ya Kanisa Kuu Ia Mt. Antoni wa Padua, Chumbageni na Mhashamu Askofu Maurus Komba aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga

TUZO ZA HESHIMA:-
Tarehe 15, Augosti, 2019, Padre Ernest Andrea Seng'enge, pamoja na Pd. Padre Martin Maganga, Pd. Odillo Mtoi, Pd. Stansiaus Baruti, Pd Severine Msemwa na Pd. Denis Mavunga walitunukiwa Tuzo ya Heshima ya utume uliotukuka yenye hadhi ya Umonsiyori (Chaplain of His Holiness) na Baba Mtakatifu Francis, iliyowasilishwa kwao na Mhashamu Askofu Anthony Banzi, Askofu wa Nne wa Jimbo Katoliki la Tanga, katika Ibada ya Misa Takatifu iliyofanyika Parokia ya Kanisa Kuu la Mt. Antoni wa Padua, Chumbageni Tanga.

SEHEMU ALIZOWAHI KUISHI NA KUFANYA KAZI KATIKA MAISHA YAKE:-
Mons. Ernest Andrea Sengenge wakati wa uhai wake, baada ya kupewa daraja la Upadre alitumwa kufanya kazi mbalimbali na kushika nyadhifa mbalimbali kama Paroko na Paroko msaidizi katika Parokia ifuatavyo:-
1981-1987:- Paroko Msaidizi Parokia ya Mt. Theresa Barabara ya 20, Tanga
1987-1991:- Paroko Parokia ya Rangwi,
1991-1997:- Paroko Parokia ya Lushoto,
1997-2021:- Kapilano (Chaplain) Nyumba ya Malezi ya Masista wa Usambara-Rangwi,
2001-2007:- Parako Parokia ya Hale,
2007-2011:- Paroko Msaidizi Parokia Tarajiwa ya Mizozwe,
2011-2013:- Mwalimu na Baba wa Kiroho Soni Seminari.
2011-2016:- Naibu Gombera Seminari ndogo ya Soni,
2016:- Msaidizi wa Paroko Parokia ya Mazinde Ngua,
2016-2022:- alishi akiendelea kupata Matibabu katika Parokia ya Kanisa Kuu Mt. Anthony Chumbageni-Tanga
2022-2024:- aliishi akiendelea kupata Matibabu katika Nyumba ya Malezi ya Wazee Neema-Tanga

UGONJWA, MATIBABU NA MAUTI:-
Mons. Ernest Andrea Seng'enge, alianza kuugua mnamo mwaka 2016 akiwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mazinde Ngua, Aliugua ghafla mnamo mwezi Septemba 2016, na alikimbizwa Katika Kituo cha Afya Kwalukonge, na ililazimika kupelekwa katika Hospital ya Rufaa KCMC-Moshi kwa uchunguzi na matibabu zaidi. Hivyo iligundulika amepata ugonjwa wa Kiharusi (Stroke). Alianza kupata matibabu kwa muda mrefu, na hali yake iliendelea kuimarika, na aliruhusiwa na kurudi nyumbani kuendelca na mazoezi. Hivyo Mons. Ernest Andrea Seng'enge aliendelea kuhudhuria Kliniki kila mwezi katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC. Baadae alianza kuhudhuria Kliniki kila baaada ya miezi mitatu. Siku ya Alhamisi tarehe 01 August, 2024, Pd. Melchiory Marandu alitoa taarifa ofisi ya Jimbo kuwa Mons. Ernest Andrea Seng'enge, anaumwa na anatapika hivyo alikimbizwa katika Kituo cha Afya Tumaini, ambapo iligundulika kuwa alikuwa akisumbuliwa na mchafuko wa Damu. Alitibiwa na kurudi nyumbani. Lakini Usiku wa tar 02 Agosti hali ilibadilika tena ghafla, na kurudishwa tena Tumaini. Pd. Paul Semng'indo na Sr. Philipina walienda usiku huo Tumaini kumwona. Madaktari wa Kituo cha Afya Tumaini walimpa rufaa ya kwenda Hospital ya Rufaa ya Bombo kwa matibabu zaidi. Alipokelewa na kulazwa kwa uangalizi zaidi. Hali iliendelea kudhoofu sana siku ya Jumamosi ya tarehe 03 Agosti,2024 saa 04:45 asubuhi, mpendwa wetu Mons. Ernest Andrea Seng'enge, Mwenyezi Mungu alimwita katika makao yake ya milele.

"Raha ya milele umpe ee Bwana, - na mwanga wa milele umuangazie
apumzike kwa Amani - Amina."

Mons. Ernest Andrea Seng'enge amefariki akiwa na umri wa miaka 75 ya kuzaliwa na miaka 43 ya utume kama Padre wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga.

MATIBABU:-
Mons. Ernest Andrea Seng'enge alipatiwa huduma ya matibabu sehemu mbalimbali kama ifuntavyo:-
Kituo cha Afya Kwalukonge, Tanga,
Hospitali ya rufaa KCMC-Moshi,
Hospitali ya Rabininsia-Dar cs Salaam,
Kituo cha Afya Tumaini-Tanga na Bombo Hospital-Tanga.

SHUKRANI:-
Mhashamu Askofu Thomas John Kiangio, askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga, pamoja na Mapadre wa Jimbo Katoliki ia Tanga, wanapenda kutoa shukrani za dhati kwa wale wole walioshiriki katika jitihada za kusaidia katika ugonjwa na kuokoa maisha ya mpendwa wetu Mons, Ernest Andrea Seng'enge.
1. Tunakushukuru sana Mama Mkuu, Sr. Gaspara Kashamba, wa Shirika la Masista wa Mama Yetu wa Usnmbara-Kwamndolwa, pamoja na uongozi mzima, kwa utayari wa kushiriki katika msiba huu na michango yenu ya hali na mali ili kufanikisha shughuli zote za mazishi ya Mpendwa wetu. Asanteni sana.
2. Tunapenda kutoa shukrani kwenu Madaktari, Wauguzi na Wafanyakazi wa Kituo chetu cha Afya Tumaini, Hospitali ya Bombo, Hospitali ya KCMC, Hospitali ya Rabininsia Dar es Salaam na Kwalukonge Health Center kwa kumhudumia kwa Moyo wa upendo Padre wetu mpendwa.

catholic diocese of Tanga

© 2024