WASIFU WAKE
+ Marehemu Msgr. Martin Jacob Pesambili Maganga alizaliwa na wazazi baba Jacob Pesambili Maganga na mama Susana Kajembe katika
kijiji cha Mwakijembe wilayani Muheza, Tanga, Tanzania.
ELIMU
1951 – 1954: Alisoma elimu ya msingi darasa la I –IV katika shule msingi Mwakijembe, Tanzania
1955 – 1959: alisoma elimu ya kati darasa la V – X huko Kwediboma Middle School, Handeni, Tanzania
1960 – 1961: alijiunga na Teacher Education huko Singachini Teachers’ College in Moshi Tanzania
AJIRA
1962 – 1963: Aliajiriwa na serekali kuwa mwalimu wa shule msingi huko Kibaranga Primary School, Kibaranga, Muheza, Tanzania
MAFUNZO YA UPADRE
1964 – 1965: Alijiunga tena na seminari ndogo kwa kidato cha III - IV huko Nyegezi Seminary Mwanza, Tanzania
1966: alifanya mwaka wa kichungaji parokiani Kongoi Lushoto, Tanzania
1967 – 1968: alijiunga na masomo ya Falsafa (Philosophy) huko Kibosho Major Seminary, Moshi, Tanzania
1969 – 1972: alijiunga na masomo ya Theolijia (Theology) huko Kipalapala Senior Seminary, Tabora, Tanzania
USHEMASI NA UPADRE
January, 1972: alipata daraja la ushemasi katika kanisa la Mt. Anthony wa Padua (Cathedral) Chumbageni, Tanga, Tanzania
June 25, 1972: alipata daraja takatifu la upadre katika kanisa la Mt. Anthony wa Padua (Cathedral) Chumbageni, Tanga, Tanzania
August 15, 2020: Received Papal honorable title MONSIGNOR in Tanga, Tanzania)
POST ORDINATION STUDIES
1975 – 1976: Diploma in Education at Chang’ombe Teachers College in Dar Es Salaam, Tanzania
UTUME WAKE JIMBONI
1972 - 1973: Mwalimu na mlezi seminari ndogo ya Mt. Peter, Morogoro, Tanzania
1974: paroko msaidizi parokia ya Mt. Theresa wa mtoto Yesu Bar.20 Tanga, Tanzania
1977 – 1981: mwalimu na mlezi seminari ndogo ya jimbo Mt. Joseph Soni Lushoto, Tanzania
1979 – 1981: Gombera wa seminari ndogo ya jimbo Mt. Joseph Soni Lushoto, Tanzania
1982 – 1984: paroko msaidizi parokia ya Kilole Korogwe, Tanzania
1985 – 1989: paroko parokia ya Mt. Anthony wa Padua (Cathedral) Chumbageni Tanga.
1989 – 1998: Chaplain at Nyegezi Social Institute in Mwanza, Tanzania.
1998 – 2006: Chaplain at St. Augustine University of Tanzania (SAUT) in Mwanza
2006 – 2008: Paroko parokia ya Mt. Agustino Manundu Korogwe.
2008 - Paroko parokia ya Mt. Theresa wa mtoto Yesu Bar.20 Tanga, Tanzania
2008 - December 19, 2020: wakili wa Askofu jimboni Tanga, Tanzania
KIFO CHAKE
Marehemu Msgr. Martin Jacob Pesambili Maganga alifariki January 13, 2021 baada ya kuugua kwa muda mfupi. Alizikwa siku ya Jumanne January 19, 2021
katika makaburi ya mapadre parokia ya Kilole Korogwe Tanga. Kifo chake kilitokea muda mfupi sana baada ya kifo cha aliyekuwa askofu wa jimbo katoliki Tanga
marehemu askofu Anthony M. Banzi ambaye alifariki Desemba 19, 2020. Msgr Maganga aliweza kudumu katika utume wa upadre kwa miaka 49.
Raha ya milele umpe ee Bwana: Na mwanga wa milele umuangazie
Apumzike kwa amani: Amina.
catholic diocese of Tanga © 2024
|