KANISA KATOLIKI TANGA
Main house

Benedictine Fathers, Sakharani Chini

Wamonaki wa Kibenedictini wa Mtakatifu Ottilien walikuja kusini mwa Tanzania tamgu mwaka 1887. Walianzisha nyumba yao huko Ndanda. Mwaka 1946 walipata nyumba ya mapumziko katika Milima ya Usambara. Sehemu hii ya Usambara ilikuwa ni shamba la Mjerumani aliyejulikana kwa jila la Sakharani ambalo lilisheheni zao la kahawa na miti ya aina mbalimbali. Eneo hili liliitwa Sakharani au Sakarani kumuenzi aliyekuwa mmiliki wa Shamba hilo:

Chaple

Wamonaki watatu waliofika mwanzoni ni Pd. Edward Wildbaher, Br. Fintan Frank na Br. Fortunatus Mayer. Hali ya hewa ya Sakharani ni baridi ambayo ni karibu sawa na ile ya Ulaya, hivyo sehemu hii ikawa sehemu nzuri ya mapumziko.

Mwaka 1970, Padre Burkad alifika Sakharani. Yeye aliomba kibali cha kufanya kazi za Kichungaji katika maeneao ya Masange na maeneo yanayoizunguka Sakharani. Aliweza kujenga Parokia ya Sakharani na vigango vyake, yaani, Kwehangala, Tekwa, Baga, Kwesine na Msamaka. Baadaye mwaka 2001 kigango cha Tekwa kilifanywa kuwa Parokia chini ya Padre Joseph Sekija. Baadaye Padre Edwin alifika na kusaidia kazi za Kichungaji.

Padre Beda Pavel alikuwa Mwalimu huko Soni Seminari wakati ilipoanzishwa. Padre Odillo Huppi alianzisha Parokia ya Handeni na utume rasmi kwa Wamasai. Padre Damian Milliken ameanzisha Shule ya Sekondari ya Wsichana Mazinde Juu na ujenzi wa Kanisa la Mabughai ambalo lina hadhi ya kuwa Parokia.

Padre Athanas Meixner alipewa jukumu la kuanzisha Parokia huko Soni na aliifanya kwa ufanisi. Pia amesaidia ujenzi wa Kanisa la Manundu -Korogwe na Kanisa la Malindi. Pia ameanzisha shamba huko Kwematuku -Korogwe.

Pamoja na kazi za Kichungaji zilizofanywa na Wamonaki hawa, kazi zao kuu hasa ilikuwa ni kilimo, ufugaji na ufundi. Walizanza kwa ujenzi wa nyumba na mabanda ya ngombe. Pia waliendeleza mashamba ya kahawa na miti ya quinine. Wamonaki hawa walisaidia sana katika ujenzi wa makina na nyumba mbalimbali za Kanisa. Br. Fortunatus atakumbukwa sana kwa mchango wake wa ujenzi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Anthony Tanga.

Katika viwanda Wabenedicti wameazisha kiwanda cha kutengeneza divai na kutengeneza mafuta ya kadamia. Pia wanayo karakana ya seremala na magari, upo ukataji wa mbao na utengenezaji wa siagi.

Wamonaki Wakibenedicti wamejitahidi sana kulea Miito ya Upadre na Kitawa. Padre Ernest Seng’enge, Padre Antony Mtunguja, Clement Kihiyo Jandu; Padre Placidus Mtunguja (OSB), Padre Cornelius Mdoe (OSB), wote hawa ni matunda ya utume wa Wabeneditini.

Sakharani chini Health post
Capentry workshop

Fr. Damian Milliken

Padre Damian Milliken

Br. Rapp
Br. C. Helbling

Fr. Burkard Shcheneider

Padre Burkad

Fr. Thomas Estermann

Padre Thomas

Fr. Athanas Meixner

Padre Athanasi Meixner