19 Machi, Sikukuu ya Mt. Yosefu Mume wa Bikira Maria Sikukuu ya somo wa Seminary ya Soni na siku ya Wazazi |
|||
|
|||
19 March, Ni sikukuu ya Mtakatifu Yosefu Mume wa Bikira Maria. Mtakatifu Yosefu pia ni Somo wa Seminary ndogo ya Soni, katika Jimbo katoliki la Tanga. Mwaka huu wa 2007 siku hii imepewa rasmi jukumu maalumu na kuitwa siku ya wazazi. Mwaka huu wa 2007 siku hii ilisherehekewa siku ya Jumamosi ya Tar. 17 Machi. Ilikuwa ni siku ya furaha kubwa sana kwa wazazi, wanafunzi na walezi kujumuika pamoja na kuwa na lengo moja la kufurahia Mungu anayowajalia katika maisha. HOTUBA YA BABA ASKOFU. Mtakatifu Yosefu anatuonesha fadhila kuu ya upendo na kutenda mema kwa yeyote yule. Alikubali kumpokea mtoto ambaye si wake na kumtunza mtoto na mama yake. Walezi wetu hapa Seminari wanawapokea wanafunzi kwa mapendo makubwa na kuwatunza bila kufahamu wazazi wao. Huku ni kufuata fadhila za Mtakatifu huyu. Wote tunahitajika kuwa watu wa Mungu, na kukubali majukumu yote tunayopewa mbele yetu, kama Mt. Yosefu. Tuombe Mungu tujaliwe na sisi kuyatunza mafumbo matakatifu, mafumbo ya ukombozi wetu, mwili na damu ya Kristo. Seminary hii ni yetu sote, Askofu, walezi, walimu, wazazi na waamini wote. Hiki ndicho kituo kinachotulelea mapandre wetu wa baadaye. Tunaamini, hata mwanafunzi asipokuwa padre basi atakuwa mkristo mwema na raia mwema kwa nchi yetu. MAFANIKIO
|
|||
|
|||
MATATIZO - Wazazi katika siku hii ya Mt. Yosefu walichangia kiasi cha pesa taslimu na ahadi, Tshs Milioni 1.5 na tani 3.5 za cement. Huu ni mchango mkubwa katika kufanikisha maendeleo ya shule yetu. Bila kuwasahau Mama wa Shauri Jema pia walichangia kama kawaida yao, mchele, sukari, mafuta na vitu vingine vingi tu. WAWATA Chumbageni pia walichangia fedha. SHUKRANI. |
|||
Imetayarishwa na Pd. Richard Kimbwi |